DKT. KIJAJI AIPA TANO BODI YA TAWA
Na, Sixmund Begashe, Arusha Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imepongezwa kwa ubunifu wake katika utekelezaji wa majukumu yake yaliyosababisha mafanikio katika uhifadhi na Utalii nchini. Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ametoa pongezi hizo leo Januari 08, 2026 Jijini Arusha wakati akipokea taarifa ya utekelezaji kazi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA inayomaliza muda wake. Dkt. Kijaji amesema ubunifu katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo, umeendana sambamba na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uhifadhi endelevu wa urithi wa rasilimali kwa maslahi ya vizazi vijavyo na Taifa kwa ujumla. Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine, Bodi hiyo imewezesha kuongezeka kwa wawekezaji na mapato kusababisha kuimarika kwa uhifadhi, kupungua kwa uvamizi katika maeneo ya hifadhi na mapori tengefu pamoja na kuimarisha matumizi y...