HUU HAPA MKAKATI WA WMA KUTOA ELIMU YA VIPIMO
KATIKA kuhakikisha elimu ya vipimo inawakia wananchi wengi zaidi Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) imedhamiria kuanzisha club za mafunzo kuhusu Vipimo katika Shule za Msingi na Sekondari kuhusu Sekta ya vipimo ili watoto wawe na uwelewa mpana kuhusu vipimo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Veronica Simba wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari walipomtembelea kwenye banda lao katika maonyesho ya 49 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea Sabasaba.
Amesema kuwa, kutokana na maoni na maswali waliokuwa wanaulizwa na wananchi kuhusu Vipimo wameona ipo haja ya kuisambaza zaidi elimu hiyo ili imfikie kila mtu kwa upana zaidi."Elimu hii inatakiwa imfikie kila mtu kwa upana zaidi na sasa tumekuja na mikakati ambayo tunatamani kwenda kuitekeleza ili sasa tufikie sehemu kubwa zaidi ya jamii"amesema Veronica .
Amesema kuwa, kwa sasa wamekua wakitoa elimu kupitia vyombo vya habari na wanashukuru kwa ushirikiano mkubwa wanaopata na elimu inayowafikia jamii.
Ameongeza kuwa, mwitikio wa wananchi umekua mkubwa sana, waliofika katika banda hilo kutaka kujua wanafanya vipi shughuli zao na ni vitu gani hasa wanavovihakiki badala ya mezani za kupimia bidhaa .
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Temeke Hilolimus Mahundi amewashauri wananchi wanapoenda kununua Nishati ya gesi ya kupikia wahakikishe ile gesi wanapimiwa kwenye mzani ambao umehakikiwa na Wakala wa Vipimo.
"Mwananchi unapoenda kuchukua gesi hakikisha kwanza usome maelekezo ya mtungi yameandikwaje na kabla hujauchukua kwenda no nyumbani hakikisha umeupima kama kweli upo sahihi,na ukiona haupo sahihi sisi kila Mkoa tuna Ofisi unaweza kutoa taarifa ili upate msaada wa kisheria"amesema Mahundi.
Comments
Post a Comment