WAZIRI DKT NDUMBARO - OFISI YA OCPD NI MUHIMU KATIKA UTUNZI NA UREKEBU WA SHERIA







Na Mwandishi wetu 

WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt, Damas Ndubambaro amesema kuwa Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) ni Taasisi muhimu sana katika suala zima la utunzi na urekebu wa sheria.

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitembelea banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria OCPD lililopo katika maonyesho ya 49 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere (Sabasaba).

Amesema kuwa, bila  Ofisi hiyo hakuna sheria ambayo inakwenda kufanyiwa marekebisho wala hakuna sheria ndogo, sheria zote zinafanyiwa marekebisho na zinatafsiriwa.

Amesema kuwa ni Ofisi muhimu sana, kwani Ofisi hiyo ikifungwa hata mahakama itakua haiwezi kufanya kazi, kwani watatumia sheria ambazo sio sahihi .

"Ni Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa sheria ndio ambayo inatuambia sheria sahihi ni hii ya mwaka huu na kwa toleo hili, lakini kwa sasa hivi wanafanya kazi nzuri za kutafsri sheria kutoka lugha ya kingereza kwenda kiswahili.

Aidha, amesema mpaka kufikia June 30 Ofisi hiyo wmeshatafsiri sheria 300 kati ya sheria 446 ambapo katika mwaka huu wa bajeti wameshatenga fedha kwa ajili ya kutafsiri sheria 146 zilizobakia ili sheria zote 446 ziwe katika lugha ya kiswahili ili watanzania waweze kuzielewa hiyo ndio kazi yao ya msingi.

"Ofisi hii ni muhimu sana Kwa ajili ya kutunga na kuchakata sheria za nchi"amesema Waziri Ndumbaro

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI