WMA YAFIKIA MALENGO MAONYESHO SABASABA

LENGO la kushiriki maonyesho ya Sabasaba limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuliko hata matarajio yetu tumekuwa na mwitikio mkubwa watu wengi wamefika katika banda letu na kutaka kujua tunafanyaje kazi kuhusu Vipimo"


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Uhusiano kutoka Wakala wa Vipimo Tanzania WMA Veronica Simba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es Salaam.

Amesema kuwa katika kuhitimisha maonyesho hayo tangu yalipoanza June 28, 2025, wamepata matokeo mazuri na kwamba wanajipanga kwa mikakati mizuri zaidi ya kutoa elimu kwa jamii.

Ameongeza kuwa, wanafanya vipimo kwenye bidhaa zilizofungashwa hadi kwenye supamaket, mfano mtu akinunua bidhaa yoyote ambayo imeshapimwa kama kahawa, mafuta ya kula yeye anajuaje kama kipimo kilichotumika ni sahihi, hilo ni jukumu la wakala wa vipimo kumuhakikishia mlaji amepewa kitu kinachoendana na ujazo uliowekwa.

Kama umechukua mafuta yamefungashwa halafu ukaambiwa ni robo lita wewe unajuaje kama kipimo kilichoandikwa kinaendana na uhalisia na kilichomo ndani hilo ni jukumu la Serikali kuhakiki kujua ukweli wa bidhaa unayoichukua na huwa tunafanya hivo"amesema Veronica 

Ameongeza kuwa, hata katika sekta ya Afya wanafanya vipimo katika mizani ya hospital ili mgonjwa atakapopewa dawa iendane na uzito wake lile ni jukumu la Serikali kuhakikisha Vipimo vile vimehakikiwa.



Pia wanahakiki mizani ya kupimia nyama, (Bucha) ili kuangalia kama zipo sahihi, na hiyo inawasaidia wote wawili mlaji na muuzaji ndio maana wanafanya uhakiki wa mizani na kuweka stika.

"Hata sekta ya kilimo tunahakiki mizani za kupimia mazao hususani mazao ya kimkakati korosho na pamaba lengo ni kumlinda mlaji na kuwalinda wafanyabiashara ili pande zote mbili zipate stahiki"

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI