Posts

Showing posts from January, 2026

DKT. KIJAJI AIPA TANO BODI YA TAWA

Image
Na, Sixmund Begashe, Arusha Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imepongezwa  kwa ubunifu wake katika utekelezaji wa majukumu yake  yaliyosababisha mafanikio katika uhifadhi na Utalii nchini.  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ametoa pongezi hizo leo Januari 08, 2026 Jijini Arusha wakati akipokea taarifa ya  utekelezaji kazi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA inayomaliza muda wake.  Dkt. Kijaji amesema ubunifu katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo, umeendana sambamba na maono ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uhifadhi endelevu wa urithi wa  rasilimali kwa maslahi ya vizazi vijavyo na Taifa kwa ujumla.  Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine, Bodi hiyo  imewezesha  kuongezeka kwa  wawekezaji na mapato kusababisha kuimarika kwa uhifadhi, kupungua kwa uvamizi katika maeneo ya hifadhi na mapori tengefu pamoja na kuimarisha matumizi y...

MAAFISA 84 NA ASKARI 48 WA TAWA WATUNUKIWA VYEO VYA UHIFADHI

Image
  Na Beatus Maganja, Morogoro Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mlage Yussuf Kabange, Januari 07, 2026 aliwatunuku na kuwavisha vyeo vya uhifadhi Maafisa 84 na Askari 48 wa taasisi hiyo, katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TAWA mkoani Morogoro. Akitoa nasaha zake kwa Maafisa na Askari hao, Kamishna Kabange aliwapongeza kwa kufikia hatua hiyo muhimu katika utumishi wa umma, huku akiwaagiza kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, nidhamu na kwa kuzingatia maadili pamoja na taratibu za kijeshi. Aidha, Kamishna Kabange alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa Maafisa na Askari wa uhifadhi kupandishwa vyeo sambamba na utoaji wa ajira mpya. Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 na 2025/2026, TAWA imepewa kibali cha kuajiri jumla ya Maafisa na Askari 550, hatua inayoongeza morali kwa wahifadhi, kupunguza changamoto za rasilimali watu,...

TUNA DENI LA KUSIMAMIA MIRADI NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO YA KWELI–MHE. SALOME

Image
  Aanza ziara ya kikazi mkoani Shinyanga kukagua miradi ya nishati Ataka changamoto za wananchi zitatuliwe kwa wakati Siku 100 za Rais Samia Umeme kuwashwa kwenye vitongoji mkoani Shinyanga SHINYANGA Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa la kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na kusikiliza pamoja  na kutatua kero za wananchi ili kufanikisha maendeleo ya kweli. Mheshimiwa Salome ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari, 2026, mkoani Shinyanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya nishati inayotekelezwa mkoani humo.  Amesema wananchi wana imani kubwa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa viongozi kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinatatuliwa kwa wakati. Ameongeza kuwa katika siku 100 za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Wizara ya Nishati imejipanga kuhakikisha umeme unawashwa kwenye miradi ya vitongoji mkoani Shinyanga ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa ...