KILO 3,182, ZAKAMATWA DAR NA IRINGA,DCEA YAFUNGUKA
Na Mwandishi wetu, Dar Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa Tanzania (DCEA) imekamata jumla ya kilogram 3,182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine katika oparesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Mkoani Iringa kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi Dicemba mwaka 2023. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mapema leo hii Kamishna Jeneral wa DCEA Aretas Lyimo amesema kuwa katika oparesheni hiyo jumala ya watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo ambapo wawili kati yao wana asili ya Asia. Amesema kuwa, kiasi hicho cha dawa za kulevya hakijawai kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya, hivyo watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani. "Kiasi hiki cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180,29 za dawa aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika Wilaya za Kigamboni, Ubu