KILO 3,182, ZAKAMATWA DAR NA IRINGA,DCEA YAFUNGUKA

Na Mwandishi wetu, Dar

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa Tanzania (DCEA) imekamata jumla ya kilogram 3,182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine katika oparesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Mkoani Iringa kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi Dicemba mwaka 2023.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mapema leo hii Kamishna Jeneral wa DCEA Aretas Lyimo amesema kuwa katika oparesheni hiyo jumala ya watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo ambapo wawili kati yao wana asili ya Asia.

Amesema kuwa, kiasi hicho cha dawa za kulevya hakijawai kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya, hivyo watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani.

"Kiasi hiki cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180,29 za dawa aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika Wilaya 

za Kigamboni, Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam pamoja na Wilaya ya Iringa mkoani Iringa"amesema Kamishna Lyimo.

Aidha, dawa hizo zilizokamatwa zilikuwa zimefungashwa kwenye vifungashio vyenye chapa mbalimbali za kahawa na majani ya chai ambapo mbinu hiyo inatumika kwa lengo la usafirishaji wake kukwepa kubainika.

Hata hivyo, amesema kuwa dawa aina ya methamphetamine ni dawa mpya ya kulevya iliyopo katika kundi la vichangamshi sawa cocaine ambapo dawa hiyo huwa kwenye mfumo wa vidonge, unga au chembechembe mithili ya chunvi ang'avu yenye rangi mbalimbali ambayo huzalishwa kwenye maabara bubu kwa kuchanganya aina mbalimbali za kemikali bashirifu.

"Dawa hii ni hatari kwa afya ya mtumiaji madhara yake ni makubwa na hayatibiki kirahisi kwani mtumiaji hupata madhara ya kudumu kwenye ubongo na hivyo hupunguza uwezo wa kutunza kumbukumbu na kusababisha uraibu na kuathiri mfumo mzima wa fahamu.

Ameongeza kuwa, kiasi cha dawa za kulevya zilizokamatwa zingefanikiwa kuingia mtaani zingeweza kuathiri zaid ya watu 76, 368,000 kwa siku hivyo, ukamataji huo umeokoa nguvu kazi ambayo ingeangamia kutokana na madhara yatokanayo na madawa ya kulevya ndani na nje ya nchi.

Sambamba na hayo DCEA imetoa onyo kwa wote wanaoendelea kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini Tanzania, huku ikiwataka wajikite kwenye biashara nyengine halali kwani mamlaka imejidhatiti kukomesha biashara hiyo kwa kufanya oparesheni katika maeneo mbalimbali nchin.

Aidha, DCEA imeishukuru Serikali ya Jamuhuri ya muunganobwa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluh Hassa kwa kuendelea kuiwezesha mamlaka hiyo katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi mkubwa.



Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI