Posts

Showing posts from January, 2024

DKT. BATILDA BURIAN AIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWA JITAHADA ZA KUKUZA UTALII MKOANI TABORA

Image
Na. Beatus Maganja Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Salha Burian ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kwa jitihada za dhati za kukuza utalii Mkoani Tabora. Dkt. Batilda alitoa pongezi hizo Januari 15, 2024 alipotembelewa na Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda ofisi kwake akiwa katika ziara ya kikazi Kanda ya Magharibi iliyokuwa na lengo la kukagua shughuli za uhifadhi na utalii zinazofanywa na TAWA Mkoani humo. Mkuu huyo wa Mkoa alisema anatambua jitihada zinazofanywa na TAWA katika kuboresha miundombinu ya utalii katika bustani ya Wanyamapori Mkoani humo ijulikanayo kama Tabora ZOO na kuishauri Mamlaka hiyo kuangalia uwezekano kuongeza miundombinu katika bustani hiyo kwa ajili ya kuongeza mapato. Vilevile, alishauri kuongeza mazao mbalimbali ya wanyamapori kama vile sumu ya nyoka ambapo alisema kuwa inahitaji utafiti zaidi. Pia Dkt. Batilda alisema ili kuendelea kuchagiza shughuli

USIKOSE KUFUATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24, ZIJAZO, LEO JAN, 19, 2024

Image
 

MVUA ZA EL - NINO NI SABABU YA ONGEZEKO LA MAMBA KASAHUNGA NA MAYOLO - DC BUNDA

Image
Na. Beatus Maganja  Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Dkt. Vicent Anney amesema mvua za El Nino zimekuwa sababu kubwa ya ongezeko la wanyamapori aina ya mamba ambao wamekuwa wakitoka maeneo yao ya asili na kwenda maeneo ya wananchi na kuleta madhara kwa maisha na mali zao katika vijiji vya Kasahunga na Mayolo Wilayani Bunda. Dkt. Vicent ameyasema hayo leo Januari 18, 2024 katika ziara ya Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA, Mabula Misungwi Nyanda iliyofanyika wilayani humo kwa lengo la kuwatembelea waathirika wa mamba na kutoa pole. "Na mwaka huu, Kamishna hali hii imeongezeka sana baada ya kuwepo kwa mvua ya El Nino ambayo imesababisha mamba kutoka katika maeneo yao ya asili kwenda kusogea kwenye maeneo ya wananchi" amesema. Akifafanua zaidi suala hilo, Dkt. Vicent amesema  mamba  wamekuwa wakisafirishwa na mikondo ya maji ya mito  kuelekea ziwani jambo ambalo limesababisha wanyamapori hao kuonekana kwa wingi katika kingo za Ziwa Victoria n

WANAOPANDISHA BEI YA SUKARI KIHOLELA KUKIONA

Image
Na Mwandishi wetu, Dar KATIKA kukabiliana na uhaba wa sukari nchini Tanzania Serikali imetoa kibali cha kuagiza sukari nje ya nchi tani 50,000 ambapo inatarajiwa kuingia Januari 22, mwaka huu pamoja na kuvifungulia viwanda vyote vinavyozalisha sukari  ili kukidhi mahitaji ya wananchi. Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Bengesi wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema sukari iliyopo nchini kwa sasa haikidhi mahitaji ya wananchi, hivyo Serikali imejipanga kuchukua hatua ili kukabiliana na changamoto hiyo. Amesema kuwa, miongoni mwa sababu zilizopelekea kuwepo kwa changamoto hiyo ni pamoja na mvua za El-nino ambazo zimenyesha mwezi Novemba na Disemba mwaka 2023 ambapo zimesababisha mashamba ya miwa kujaa maji na miundombinu hivyo kupelekea uzalishaji mdogo wa miwa. Katika hatua nyengine Bodi ya Sukari Tanzania imewataka wafanyabiashara wanaouza sukari kuacha tabia ya kujipangia bei hali  inayopeleke
Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akifanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Mhe. Demeke Mekonnen Hassen. Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi. Tarehe 16 Januari 2024. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Plastic Action Partnership Bi. Clemence Schidm. Mazungumzo hayo yamefanyika kando ya Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi. Tarehe 16 Januari 2024. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Plastic Action Partnership Bi. Clemence Schidm mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika kando ya Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi. Tarehe 16 Januari 2024. Na Mwandishi wetu,

KAMISHNA WA TAWA AZINDUA MRADI WA JENGO LA OFISI LENYE THAMANI YA ZAIDI YA TZS MILIONI 250, AMPONGEZA RAIS SAMIA

Image
  Na. Beatus Maganja  Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania - TAWA amezindua mradi wa jengo la ofisi lenye jumla ya vyumba 8 vikiwemo vyumba 6 vitakavyotumika kama ofisi, chumba cha mikutano, stoo pamoja na vyoo viwili, mradi unaotajwa kugharimu zaidi ya Tsh. Millioni 250. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa  jengo hilo iliyofanyika leo Januari 16, 2024 Makao Makuu ya Ofisi za Pori la Akiba Moyowosi zilizopo Kifura wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, Kamishna Mabula amemshukuru Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiwezesha taasisi hiyo kukamilisha mradi huo na miradi mingine ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa TAWA. "Tunamshukuru Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya kazi nzuri ya kutupatia fedha zilizotuwezesha kukamilisha mradi huu na miradi mingine tunayoitekeleza ikiwa ni pamoja na mishahara, yote hii ni matokeo ya Serikali yetu, ndiyo inayotuwezesha" amesema. Aidh

TANZANIA YAPOKEA MELI KUBWA YA WATALII, MABORESHO YA BANDARI YAZAA MATUNDA

Image
Na Mwandishi wetu, Dar Tanzania kupitia Mamlaka ya Bandari TPA imeweka historia kwa kupokea meli kubwa ya watalii ikitokea nchini Norway inayomilikiwa na kampuni ya Norwegian Cruiseline Holdings ya Marekani, yenye urefu wa mita 294 ambapo meli hiyo ni ya kwanza kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1964. Hatua hiyo imekuja mara baada ya maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika katika bandari ya Dar es Salaam kupitia mradi wa maboresho ya bandari ya Dar es Salaam (DMGP) ambayo yamechagia ujio wa meli hiyo, hali  itakayopelekea kuongezeka kwa watalii nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea meli hiyo iliotia nanga majira ya saa 11 alfajiri mapema leo hii, Mkurugenzi Mkuu wa Bandari hiyo, Mrisho Mrisho amesema kuwa,malengo ya bandari hiyo ni kuhudumia meli zenye urefu wa mita 305 hadi 350.  Amesema kuwa, meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 4700 lakini kwa Tanzania wamekuja wageni zaidi ya  2000

KAMISHNA MABULA AFANYA UKAGUZI WA KARAKANA YA KISASA MANYONI, ATOA MAELEKEZO MAHSUSI

Image
Na. Beatus Maganja  Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda ameeleza kufurahishwa kwake na ubora wa viwango vya ujenzi wa karakana ya matengenezo ya magari na mitambo iliyojengwa Kanda ya Kati ya TAWA wilayani Manyoni, karakana inayotajwa kuwa ni kubwa kuliko karakana zote zilizojengwa na taasisi hiyo. Ameyasema hayo  Januari 14, 2024 akiwa katika ziara yake Makao Makuu ya Kanda ya Kati ya TAWA wilayani Manyoni, ziara yenye lengo la kukagua shughuli za uhifadhi na utalii zinazotekelezwa na TAWA wilayani humo. "Nimetembelea na kukagua karakana, kimsingi nimeona imejengwa vizuri na pia nimeona ina uwekezaji mkubwa wa vifaa vitavyotumika na nina imani hii karakana itatusaidia sana" amesema Akibainisha sababu za kuifanya karakana hiyo kuwa kubwa wilayani humo, Kamishna Mabula amesema Manyoni ni katikati ya nchi na ni sehemu inayofikika kwa urahisi, hivyo kutokana na ukubwa wake itatumika kutengeneza magari si tu ya Kanda ya Kati bali ya taasisi nzima. Aidha, Kamishna

USIKOSE KUFATILIA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24, ZIJAZO, JAN 12, 2024

Image
 

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UVIKO PORI LA AKIBA WAMI MBIKI

Image
Na. Beatus Maganja Kamati ya kudumu ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii imeeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa miradi ya mpango wa Taifa wa  maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO - 19 iliyotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ndani ya Pori la Akiba Wami Mbiki Mkoani Pwani. Akizungumza mara baada ya kutembelea na  kukagua miradi hiyo,  Mwenyekiti wa Kamati  Mhe. Timotheo Mzava amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ubunifu wake wa kutafuta fedha na maelekezo aliyoyatoa juu ya matumizi ya fedha za UVIKO ambazo zimeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii. "Kwa mazingira na hali tuliyoiona (Pori la Akiba Wami Mbiki) nadhani tutaungana sote kumpongeza kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye Nchi yetu lakini hasa kwa ubunifu mkubwa alionao wa kutafuta fedha lakini pia maelekezo aliyoyatoa Juu ya ma