AKIBA BENKI YAFUTURUSHA WATEJA WAKE, YAJIPANGA KUBORESHA HUDUMA

 

Na Mwandishi wetu,

Mkurugenzi wa Akiba Commercial Benk (ACB) Silvest Arumasi amesema kuwa ACB inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo ya kukidhi matarajio ya wateja.


Aidha, amewaomba wateja wao na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo ambayo imeweza kuwahudumia watanzania wengi na kuleta maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na Jamii nzima kwa ujumla. 

Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati akihutubia wateja na wanachama wake katika hafla maalum ya kufuturisha kwa lengo la kuwa nao zaidi katika kuwapa huduma zilizobora.

Hafla hiyo iliyofanyika tarehe 25 Machi, 2024 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa ACB  Silvest Arumasi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Waislamu wote kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na amewashukuru wadau wote kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika Futari hiyo kwani kwa kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa kwa Benki.

Aidha, amesema kuwa, ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono Waislam wote katika funga yao na pia ni njia nzuri ya kuboresha mahusiano ya benki na wateja wake.

"Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu sana Imani za wateja, Wafanyakazi na wadau wake na kuupa umuhimu wa kipekee katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan".

"Akiba Commercial BankBenki kwa maendeleo yako".

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI