BENKI YA AKIBA YATOA ELIMU YA FEDHA KWA WADAU MBALIMBALI


Na mwandishi wetu, matukio Daima

Benki ya Akiba imesema itaendelea kuunga mkono Serikali kwa kutoa elimu ya fedha huku ikiboresha huduma zake nchi nzima ili kusaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchochea  kukua kwa  uchumi wa Taifa.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba Silvest Arumasi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya elimu ya fedha yaliyojumuisha viongozi wa benki hiyo, watumishi kutoka Wizara,  taasisi na ofisi mbalimbali za Serikali lengo likiwa ni kubadilishana ujuzi na kujenga mahusiano mazuri huku wakifahamiana na kuweka mikakati ya pamoja namna ya kuwahudumia watumishi wa Umma kwa weledi zaidi na kujibu maswali na kujibu maswali huku wakitatua kero zinazojitokeza kiutendaji.

Mkurugenzi Arumasi amebainisha kuwa benki hiyo itawaangalia wananchi wa Dodoma kwa upekee kutokana na fursa mpya zilizopo katika Jiji hilo kwani serikali  imekuwa ikiendeleza na kustawisha Makao makuu ya Nchi hivyo ametoa rai kwa wananchi  kujishughulisha na biashara na wanapokwama benki hiyo ipo kutoa  mikopo kwa riba nafuu .

"Tunaahidi kuwa benki itaendelea kuunga mkono serikali kwa kuwasadia wananchi kuwapatia mikopo nafuuu  ili kuinua mitaji yao pia kupanua wigo wa huduma nchi nzima ili kufikia azma ya kutoa mchango mkubwa  wa kuwepo kwa huduma shirikishi za kifedha yaani financial inclusion" amesema Arumasi

Kwa upande wake, Upendo Makula,  ambae ni Meneja wa Tawi la ACB - Dodoma  aliwashukuru sana washiriki wote kwa kuitikia mwito  kwa ujumla wao. 

Aidha washiriki wote waliishukuru Benki ya Akiba kwa mada nzuri za semina hiyo na wameahidi kutumia elimu hiyo kama chachu katika utendaji wao wa kila siku kwani wamejengewa    msingi imara  wa uelewa wa maswala ya fedha.


Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI