JUMIKITA :SERIKALI ISIINGIE KWENYE MTEGO WA KUFUNGIA MTANDAO WA 'X ' ZAMANI TWITTER


Baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake  Mohammed Ali Kawaida kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter kutokana na mtandao huo kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na Utamaduni wa Watanzania 

Leo Juni 12,2024, Jukwaa la wanahabari wa mitandao ya Kijamii Tanzania(JUMIKITA) likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Ndg.Shabani Matwebe limeiomba Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Uongozi makini wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao huo wa Kijamii 

"Ni kama ilivyo Instagram  ,Facebook na YouTube, 'x' au Twitter  ni sehemu ambayo vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia Jukwaa hilo kujipatia riziki mfano Matangazo lakini pia hata Kazi nzuri za Serikali mbalimbali Wanahabari wa mtandaoni wamekua wakizichapisha 'x' "

Taarifa ya Jukwaa imeongeza kua

"JUMIKITA ipo tayari kushirikiana na Serikali kujua namna bora ya matumizi  ya mitandao ya kijamii na inatoa ushauri serikali isiingie kwenye mtego wa kufungia mtandao huo"

 _Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA)_

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...