Posts

Showing posts from July, 2024

NAIBU SPIKA WA BUNGE ZUNGU MGENI RASMI MAHAFALI YA 19 YA CHUO CHA FURAHIKA.

Image
  Na Mwandishi wetu, Habari Plus  Naibu Spika la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu anatarajiwa kuwa mgeni ya rasmi katia mahafali ya 19 ya Chuo Cha Ufundi Stadi cha Furahika ambacho kipo Buguruni Malapa jijini Dar Es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya amewaomba wazazi na walezi wa vijana hao wanahitimu na wengine kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo muhimu katika maisha ya watoto wao. Amesema kuwa, mahafali hayo yatafanyika Agosti 3 mwaka huu na wahitimu 120 wa kozi mbalimbali ikiwemo Ualimu, Sekretari, Hotel na nyinginezo ambazo zipo chini ya Veta na mhitimu ambaye amefanya vizuri kwa kila kozi atapewa zawadi kama ilivyo kawaida. "Tunayofuraha kubwa  kwenda kusheherekea mahafari ya 19 tangu chuo hiki kianzishwe na mgeni wetu ataakuwa Mbunge wa Ilala, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mussa Zungu, hivyo tunawaomba wazazi ama walezi wa vijana ambao

WALIMU ZAIDI YA 1000 KUPANDA SGR KWENDA MIKUMI

Image
Na Mwandishi wetu, Habari Plus Zaidi ya walimu 1000 kupanda Treni ya Umeme SGR kwenda Hifadhi ya Taifa Mikumi-Morogoro, lengo ni kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kufuatia uwekezaji mkubwa alioufanya katika usafiri wa reli ya SGR Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa taarifa kwa umma juu ya uzinduzi wa Treni ya SGR ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Dodoma Agosti 01,2024  Aidha, RC Chalamila amesema ofisi yake imeandaa Safari SGR Mikumi Tour kwa walimu wa Mkoa huo, ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti 02,2024 siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kufanya uzinduzi wa SGR Mkoani Dodoma. Hata hivyo, amesema program hiyo inaanza kufanyika kwa kundi la walimu Zaidi ya 1000 na itaendelea kufanyika kwa makundi mengine kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt Samia kutokana n

DKT. BITEKO AWAKEMEA WATUMISHI WANAOKWAMISHA WAFANYABISHARA

Image
  Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka watumishi Serikalini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na misingi ya utoaji wa huduma ili kuleta matokeo Chanya na sio kuwakwamisha watu wanohitaji huduma. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo (Julai 30,2024) wakati akizindua Sera Taifa ya Biashara katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Serikalini na sekta binafsi. Amesema katika baadhi ya ofisi kuna watu mahiri wa kuandaa maandiko lakini utekelezaji wa majukumu yao hauna uhalisia na hauendani na nyaraka walizoziandaa na hivyo nyaraka hizo kubaki kwenye makablasha. “ Tunaweza kuwa wazuri sana wa kuandika kutoa matamko na kutoa ahadi lakini hali halisi haibadiliki, Hakuna faida ya kuwa na afisa anayejipanga kumkwamisha mfanyabiashara ili tu aitwe bosi, Tunatakiwa kuwa na nyaraka inayotuunganisha wote vinginevyo sera hii itabaki kuwa kitabu cha hadithi kwenye kabati,” Am

BATA LA MSITUNI FESTIVAL KUFANYIKA PUGU KAZIMZUMBWI, DC MAGOTI AELEZEA

Image
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani Petro Magoti amewataka watanzania kushiriki kikamilifu katika tamasha kubwa la Msituni maarufu kama "Bata Msituni Festival" lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia katika kutangaza utalii wa Tanzania. Aidha, tamasha hilo linatarajia kuwakutanisha watu 3000 kutoka ndani na nje ya nchi ambapo mpaka sasa nchi tatu zimeshathibitisha kushiriki katika tamasha hilo na nyengine zinajiorodhesha ambapo pamoja na mambo mengine watu wataweza kupata burudani za kutosha kutoka kwa wasanii mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari wilaya ya kisarawe  katika hifadhi ya msitu wa mazingira asilia Pugu  Kazimzumbwi ambao unasimamiwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ambapo amesema  tamasha hilo kwa mwaka huu litakuwa ni la kipekee kwani watanzania watapata fursa ya kukaa katika msitu huo kwa takribani siku sita wakifurahia maisha na mandhari ya msitu huo.  "Msitu huu hauna wanyama wakali ba

NAIBU WAZIRI MKUU DKT BITEKO MGENI RASMI UZINDUZI WA SERA YA TAIFA BIASHARA 2003 TOLEO LA 2023

Image
  Na mwandishi wetu, HabariPlus, Dar  Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Seleman Jafo amesema kuwa miongoni mwa mafanikio yaliopatikana katika sera ya taifa ya biashara mwaka 2003 toleo la 2023 ni Serikali kufanikiwa kushiriki kikamilifu katika majadiliano mbalimbali ya biashara baina ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa kwa lengo la kuongeza fursa zaidi za biashara ya bidhaa na huduma kutoka Tanzania ikijumuisha kupata masoko yenye masharti nafuu kwa ajili ya wafanyabiashara wa Tanzania. Akizungumza na waandiahi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Tanzania imefika mauzo ya nje Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika yameongezeka kutoka shilingi trilioni 2.607 mwaka 2016 hadi shilingi trilioni 4.422 mwaka 2023, na mauzo nje kwenye Jumuiya ya Ulaya yameongezeka kutoka shilingi trilioni 0.605 mwaka 2016 hadi shilingi trilioni 3.835.65 mwaka 2023, huku bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni za kilimo, hususan kahawa, chai, mahindi, ngano, mchele, mbogamboga na bidhaa za viwandani. Amesema

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOTENDA UHALIFU, WAMO WANAOSAMBAZA JUMBE ZA UONGO WATOTO KUTEKWA

Image
Na Mwandishi wetu, HabariPlus Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani imesema Serikali haikubaliani na vitendo vyote vya kihalifu wanavyofanyiwa baadhi ya watoto, huku akiahidi hatua kali zitachukuliwa kwa yoyote atakaebainika kutenda vitendo hivyo. Aidha, Serikali haitowafumbia macho baadhi ya watu wanaotumia fursa hiyo kusambaza jumbe za uongo kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mbaimbali na kuleta taharuki ndani ya jamii. Kauli hiyo imetolewa jinini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamadi Masauni wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari alipokua akitoa taarifa ya matukio ya vitendo vya ukatili na utekaji wa watoto kwani sio tu vitendo viovu bali vinaenda kinyume na utamaduni wa Taifa lenye utu, ustaarabu, amani na utulivu. Amesema kuwa, Serikali imechukua hatua stahiki kwa wale wote waliobainika na itaendelea kuwachukulia hatua wale watakaobainika kuhusika na matukio hayo ya kihalifu, hivyo wanaungana na Rais Dkt Samia, wazazi na walezi kuke

UTABIRI WA HALI HEWA KWA SAA 24, ZIJAZO

Image
 

WANANCHI RUFIJI WAISHUKURU TAWA KWA KUWAOKOA DHIDI YA ATHARI ZA KUCHEPUKA KWA MTO

Image
Na. Beatus Maganja  Wananchi wa Kijiji cha Ngarambe, Kata ya Ngarambe wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani wameishukuru Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kwa msaada wa kuchepusha mto  uliobadili uelekeo wake  kutokana na mvua nyingi zilizonyesha Mwaka huu zikiambatana na kimbunga HIDAYA na kusababisha  uelekeo wa Mto kuelekea katika makazi na mashamba ya wakazi wa Kijiji hicho na kusababisha uharibifu wa mashamba na makazi ya wananchi hao. Wananchi hao wametoa shukrani hizo Julai 26, 2024 kwa TAWA kupitia uongozi wa Pori la Akiba Selous Kituo cha Kingupira kwa kutoa mashine inayosaidia kuchepusha mto huo kutoka makazi ya watu, jambo ambalo wamekiri kuwa litasaidia kuokoa maisha ya watu na mali zao. Salum Kassim ambaye ni  mkazi wa Kijiji cha Ngarambe amesema mvua kubwa zilizonyesha Mwaka huu ambazo ziliambatana na kimbunga HIDAYA zilisababisha athari kubwa kwa wakazi wa Kijiji hicho kama vile kuharibu makazi yao kwa kubomoa nyumba, kuharibu majengo ya shule na vyoo vya shule

MAADHIMISHO YA SIKU YA HOMA YA INI KITAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM

Image
  Na Mwandishi wetu, HabariPlus Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Chalamila awataka wakazi wa Mkoa huo na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya homa ya Ini yatakayofanyika Julai 25 hadi 28,2024 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  RC Chalamila amesema mkoa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya ngono na Homa ya INI pamoja na Halmashauri zake tano na wadau mbalimbali wa maendeleo watafanya maadhimisho ya siku ya Homa ya INI kitaifa ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika katika Mkoa huo. Aidha RC Chalamila amesema maadhimisho hayo yanakusudia kutoa elimu na uelewa wa pamoja juu ya ugonjwa wa Homa ya INI pamoja na kutoa huduma mbalimbali za Afya ikiwemo huduma za Homa ya INI kama upimaji wa maambukizi ya virusi vya Homa ya INI, Chanjo za homa ya INI pamoja na huduma zingine za Afya  na magonjwa mengine. Hata hivyo, amesema katika kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika katika viwanja vya sin

RC CHALAMILA AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NA KUWAENZI MASHUJAA

Image
Na Mwandishi wetu, HabariPlus Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu katika jiji hilo, huku akiwataka kuwaenzi mashujaa wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo. Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa wa Tanzania katika eneo la mnara wa mashujaa mnazi Mmojq ilala jijini Dar es Salaam. Aidha RC Chalamila amesema siku ya mashujaa ina umuhimu mkubwa katika historia ya Tanzania na kusema kuwa njia bora ya kuwaenzi mashujaa hao ni kuendelea kudumisha Amani na kuepuka viashiria vyote vya uvunjifu wa amani. Amesema kuwa,  muasisi wa Taifa la Tanzania Hayyt Mwl Julius K Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayyat Abeid Karume hao wamekua mfano mzuri wa kuigwa kila inapoazimishwa siku ya mashujaa kwani amani iliyopo imetokana na misingi imara walioiweka. "Kila ifikapo Julai 25 tunaadhimisha siku hii kwa kuwakumbuka wapigania uhuru mbalimbali wa taifa hi

KAMPENI YA KILIMO NI MBOLEA KUCHOCHEA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA, USAJILI WA WAKULIMA.

Image
  Na Mwandishi wetu, Ruvuma. Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imesema matumizi sahihi ya mbolea katika uzalishaji wa mazao ni muhimu kwa lengo la kurutubisha na kuboresha afya ya udongo ili kuweza kuzalisha mazao kwa wingi kati eneo dogo.  Kauli hiyo imetolewa Wilayani Mbinga na Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka hiyo Joele Laurent alipozungumza na kusanyiko la wakulima wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya TFRA ijulikanayo kwa jina la KILIMO NI MBOLEA, yenye lengo la kuhimiza matumizi sahihi ya Mbolea na kuhamasisha wakulima kujisajili na kuuhisha taarifa zao kwenye mfumo wa Mbolea ya ruzuku, ili waendelee kunufaika na mpango huo. Mkurugenzi huyo amesema, idadi ya watu inaongezeka kila kukicha hivyo matumizi sahihi ya mbolea shambani ni muhimu ili kuongeza tija na kutosheleza mahitaji ya chakula kukidhi idadi ya watu iliyopo. Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ukuaji wa miji, miundombinu na huduma nyingine za kijamii unapunguza eneo linalofaa kwa kilimo na hivyo eneo linalobaki

GRAND GALA KUNOGESHWA NA WAZIRI NDUMBARO SUPER DOM MASAKI

Image
  Wadau mbalimbali wa tansia ya muziki wa danzi wametakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 30 mwezi wa nane 2024, jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Super dom bapo nyimbo mbalimbali zitapigwa za mziki wa zamani na kizazi kipya. Aidha, Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Damas Ndumbaro anatarajia kuwa mgeni Rasmi kwenye Tamasha la Gland Gala Dance lotakalofamyika Superdome Masaki jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es asalaam  Mkurugenzi wa Chocolate Princes Mboni Masimba ambaye ndiye mwandaaji wa tamasha hilo amesema kuwa siku hiyo itakua ni siku ya kipekee kwa wadau wa tansia hiyo kuweza kupata burudani mbalimbali. Masimba amesema tamasha hilo litafanyika Agosti 30, Mwaka huu ambapo miongoni mwa wasanii watakaoburudisha ni Pacho Mwamba, Charlez Baba na wengine wengi. Kwa upande wake Pacho Mwamba amewaita watu wengi kujitokeza kwenye Tamasha hilo wakiwemo wanamuziki wa Tanzania ili weweze kujifunza mengi ikiwemo namna ya kuimba "live".

RC CHALAMILA AONGOZA KIKAO CHA BODI YA BARABARA NA KAMATI YA USHAURI YA MKOA

Image
#Atoa maelekezo mahususi juu ya ufanisi na utekekelezaja wa miradi ya barabara katika Mkoa. #Ataka kuwa na ubunifu wa matumizi ya ‘Road Reserve’ na maeneo ya wazi. #Asema Dar es Salaam ni salama sana vitendo vichache vya kiharifu vimeendelea kudhibitiwa. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 24,2024 ameongoza kikao cha bodi ya barabara na Kamati ya ushauri ya Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazi mmoja -Ilala. RC Chalamila akiongoza kikao hicho alipata wasaa wa kusikia michango na ushauri kutoka kwa wajumbe wa kikao hicho ambao ni waheshimiwa wabunge na wataalam wengine ambao walihudhuria kikao na baadaye Mhe Mkuu wa Mkoa aliwahakikishia wajumbe kulipatia suluhu tatizo la ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi ya barabara hususani ile ambayo tayari ilishatangazwa kutekelezwa, kwa hatua ya awali amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kuratibu timu ya watu wachache kwa ajili ya kwenda kumuona waziri mwenye dhamana. Aidha RC Chalamila ameagiz

WAPANGAJI WA NYUMBA ZA TBA, KULIPA KODI NI WAJIBU: WAZIRI BASHUNGWA

Image
  Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa(Mb) amewataka Wapangaji wanaokaa kwenye nyumba na majengo ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi ya pango ili fedha hiyo itumike kujenga majengo mapya na kuboresha huduma katika majengo mengine ya Wakala huo. Bashungwa ametoa agizo hilo leo Julai 23, 2024 katika hafla ya ufunguzi wa jengo la makazi ya watumishi wa umma la Magomeni Kota Awamu ya Pili B la ghorofa saba katika Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mkoani Dar es Salaam. “Serikali itaendelea kufanya kila jitihada za kujenga makazi bora ya watumishi, lakini Watumishi mliopata fursa ya kukaa kwenye nyumba za TBA, kulipa kodi ni wajibu. Mkilipa kodi inatupa uwezo wa kuboresha huduma ya makazi bora”, amesisitiza Bashungwa. Bashungwa ameielekeza TBA kusimamia ukusanyaji wa madeni kwa wadaiwa sugu kulingana mikataba waliyojiwekea ili kodi hizo ziweze kukamilisha ujenzi wa jengo la tatu na nne (Block C na D) yanayoendelea katika eneo la Magomeni ambapo utekeleza

BUKOMBE WAISHUKURU SERIKALI KWA MAENDELEO

Image
#Wajivunia ujenzi wa miundombinu huduma za jamii. #Dkt. Biteko Asisitiza umuhimu wa ushirikiano kuleta maendeleo. #Ataka Wananchi kuchagua Viongozi Wenye Sifa Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa heshima kubwa aliyowapa Watu wa Bukombe kwa kuwaletea Maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa wa hadhara katika Uwanja wa Lyambamgongo Center iliyopo Kata ya Lyambamgongo, Jimbo la Bukombe mkoani Geita. “ Nataka niwambieni mambo mazuri yanakuja, Mama Samia amesema anataka aione Bukombe mpya na mimi nawahakikishieni itabadilika Lyambamgongo haikuwa hivi na ninyi ni mashahidi lakini Rais wetu ametuletea huduma mbalimbali za maendeleo na leo tumepata barabara ya kutoka Lyambamgongo hadi Ifunde, Ishoro, Nyamakungu, hatukuwa na Zahanati leo tumepata Zahanati na Nishati ya umeme wa uhakika