KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI NLD ASISITIZA WATAFANYA KAMPENI ZA BUSARA ZA



Na Ombe kilonzo Zanzibar

Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Ahmed Salim Hamad, akizungumza katika kikao cha ndani na viongozi wa chama hicho kutoka Chaani, Zanzibar, alisisitiza kuwa kampeni za chama hicho zitaendeshwa kwa njia ya amani. Mhe. Ahmed aliwataka viongozi wa NLD Zanzibar kuongozwa na busara wanapoeneza sera na itikadi ya chama cha NLD, 

Alisisitiza, "Chama cha NLD kitaendesha kampeni za busara, kuepuka uchochezi, udanganyifu, au vurugu, na badala yake tutaweka msisitizo kwenye hoja na sera, kwani NLD Ina sera nzuri kuliko chama chochote nchini."

Aliwahimiza viongozi wa NLD kuhakikisha wanajenga mahusiano bora na wananchi wa ngazi za chini, akiwataka viongozi hao kuelewa matatizo ya wananchi na kuonyesha suluhu ya matatizo kupitia sera za chama cha NLD. "NLD haitaki kuwa kama vyama vingine vinavyolalamika bila kutoa njia za kutatua matatizo ya wananchi." Alisema Mhe. Ahmed.

Chama cha NLD kipo kwenye Ziara ya siku nne visiwani Zanzibar, inayoongozwa na Katibu Mkuu wa NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, Ziara hiyo inashirikisha viongozi wakuu wa chama hicho, na inahusisha ujenzi na kuimarisha wa chama kwenye ngazi za uongozi unaotokana na chama hicho.



Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI