SAVE THE CHILDREN WAJA NA MPANGO KAZI KWA ASASI ZA KIRAIA NCHINI TANZANIA



Na Mwandishi wetu 

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia Wazee na Watoto Dr Seif Shekalage amesema kuwa katika kufikia malengo ya miradi inayoanzishwa ni muhimu kuwashirika wananchi na kujua vipaumbele vyao ndani ya jamii hapo ndipo matokeo mazuri na endelevu ya miradi yatakapopatikana.



Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizundua mpango kazi wa Ujanibishaji (Localization) ulioandaliwa na Shirika la Save the Children uliolenga kufanya juhudi za maendeleo kwa kuwafikia moja kwa moja watoto hususani wenye mahitaji kwa kuzijengea uwezo asasi za kiraia nchini Tanzania. 

Aidha amezitaka asasi za kiraia nchini Tanzania kuwa waadilifu, wawazi kuwa na nidhamu ya pesa zinazotolewa na wafadhili kwa ajili ya usimamizi wa miradi, huku akiwataka kufanya miradi inayoendana na pesa zinazotolewa kwani kufanya hivyo, kutawajengea imani ya kupewa miradi mingine kusimamia.



Hata hivyo, amesema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan umeona umuhimu wa kuwekeza, imeanzisha idara maalum ya watoto katika usimamizi wa sera na sheria huku akiweka elimu bure , ameboresha sekta ya Afya, matibabu bure kwa watoto lengo la kuwaanda kwa Taifa la kesho.

Sambamba na hayo amewataka watoto kuzingatia maadili mwema wanayofundishwa na wazazi wao, pamoja na kuzingatia masomo Yao na kujiepusha na yake yote yatakayo badilisha ndoto zao, huku akiwataka watumie mafunzo wanayopewa kwenye miradi hiyo ili kuweza kutambua haki zao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa usimamizi wa miradi, Shirika la Save the Children Tanzania Anatory Ruge, amesema lengo la kukutana ni kuzindua mpango kazi wa Ujanibishaji (Localization) ambao unalenga kufanya juhudi za maendeleo ziwe na umiliki na ushawishi kwa wale ambao wanamahitaji husika kwa jamii husika sambamba na kuzijengea uwezo asasi za kiraia zilizopo nchini Tanzania zilizoanzishwa na watanzania ili ziwe na uongozi thabiti na sera za uwazi zinazochoche uwazi katika rasilimali pesa.

Aidha, amesema Save the Children wanahakikisha wanawajengea uwezo wadau wao ikwemo Serikali ambapo ndio mdau namba moja,  Save the Children ni washiriki na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali hivyo  wanahakikisha kwamba juhudi zao za maendeleo zinamfikia kila mtoto na kumjengea mazingira salama ya kiafya kiulinzi, kielimu katika haki zake kama mtoto.


Ameongeza kuwa, mashirika yasiyo ya kiserikali yamekua yakikumbwa na changamoto ya rasilimali pesa na kasumba ya kufikiri kwamba asasi za kiraia hawana uwezo wala mifumo inayoweza kusimamia kwa udhibiti pesa za wafadhili zinazoletwa kuweza kuwafikia walengwa wanaowahudumia.

"Save the Children ili kuondoa dhana hiyo tunataka kuweka uwaminifu na uwazi na kuona kwamba kama ni shirika basi linapaswa kua na mifumo ya utawala, iwe na bodi ambayo ni huru, uongozi pia na liwe na mfumo wa usimamizi wa kipesa ambayo iko wazi na watumishi wenye utaalam na maadili"amesema Ruge.


Naye, Sofia Lehela ambae anafanyakazi na Shirika la watoto Zanzibar, amesema asilimia 70 ya pesa ambazo zimetolewa na Save the Children zinawafikia wao moja kwa moja jambo ambalo limepekea kupata matokeo chanya ya mradi huo ikiwa ni pamoja na kuwaingiza watoto kwenye bajeti ya Serikaki, kupata muongozo mpya kwenye mabaraza ya watoto na kupata ofisi watoto kuweza kufanyia shughuli zao.

Amesema kuwa, changamoto kubwa kwa watoto Tanzania nzima ni vitendo vya ukatili na udhalilishaji dhidi ya watoto wenyewe ambapo wamejikita katika kuwangea uwezo kutetea haki zao na hata wanapokutana na viongozi wa Serikali kuwaelezea changamoto zao, watoto wao wenyewe wakijinda na kujua haki zao itapelekea kupata viongozi bora ambao wamepita na wameshiriki michakato ya kisera katika ngazi mbalimbali.



Mratibu Taifa Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu Tanzania Olesmo Olengurumwa amesema ipo haja kwa Serikali kuona umuhimu wa kuboresha sera na sheria za nchi ili ziweze kuongoza vizuri utaratibu wa kufanya ujanibishaji ya mkradi ambayo inatoka nje, pamoja na kuboresha utendaji kazi na uwezo.

Aidha, amesema, endapo pesa zinazotolewa na Nchi zilizoendelea kwa ajili ya kusaidia asasi za kiraia nchini Tanzania kusimamia miradi, zinachukuliwa na mashirika makubwa hasa ya nchi hizo zinazotoa misaada hakutakua na ukuaji wa sekta ya asasi za kiraia jambo ambalo litapelekea asasi hizo kushindwa kujiendesha na kupelekea kuondoka katika sura ya sekta ya asasi za kiraia Tanzania.


Amesema kuwa, Shirika la Save the Children linafanya kazi na watu chini, linawajengea uwezo ambapo wameamua kuja wa Ujanibishaji (Localization) mpango wa kufanya kazi na asasi za kiraia za chini kwao wao ndio ambao wanajua hali halisi ya watu wanaoishi nao ndani ya jamii na wao ndio wanajua watanzania wanataka kipi na kipi hawataki.

Sambamba na hayo, amesema akitoa takwimu za mwaka 2020 zi mwakilishi kutoka SIDA amesema asilimia 90 ya pesa zinazotengwa na nchi zilizoendelea kwa ajili ya asasi za kiraia nchini Tanzania zinachukuliwa na mashirika ya kimataifa, ambapo mengi yakitoke kwenye nchi ambazo zinatoa misaada hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Save the Children Tanzania, Angela Kauleni, amesema  wameamua kuja na mpango kazi huo wa kuzishirikisha asasi za kiraia nchini kuwajengea uwezo ili kuweza kuwafikia walengwa (wanufaika) moja kwa moja kutokana na kurithi kwa vitendo vya ukatili wa watoto hasa vijijini, kwani wao peke yao hawawezi kuwafikia kwa wingi.

"Asilimia 75 ya pesa tulizozipata kutoka mfadhili wetu SIDA tumezipeleka kwa asasi za kiraia za kitanzania saba ili zikasinamie mpango kazi huu na kupata matokeo makubwa na asilimia 25 zilizobaki zimetumika katika mambo mbalimbali ya Shirika ikiwa ni pamoja na kutekeleza mradi huu ambao umezinduliwa leo"amesema Angela.



Ameongeza kuwa, kwa kufanya hivyo wamekua na matokeo Chanya na mapinduzi makubwa sana kwenye ikiwa ni pamoja na kusimamisha mabaraza ya watoto ambayo yanawapa fursa ya kukusemea mambo yao, pia wamesukuma sera mbalimbali, wamezuia mimba za utotoni na wamefanya kazi na Serikali ambapo wamefanya uchechemuzi wa mambo mbalimbali .

Hata hivyo, wanawajengea uwezo watoto wenyewe wajiseme katika mabaraza waseme nini kifanyike na wanachangamoto zipi wana mawazo mazuri sana na wameyapokea na wanatushauri waende maeneo yapi na wanapata mabadiliko chanya mtoto hata mmoja asichwe nyuma ndio lengo kubwa la mradi.



"Tunazijengea uwezo asasi za kiraia ili ziweze kuwasaidia watoto hasa vijijini ambapo kwa asilimia kubwa ndipo vitendo vya ukatili wa kujinsia vinaripotiwa huko, na wafanye program nzuri ambazo zitakwenda kuwaondolea maumivu, kwani program nyengine zinawaumiza watoto, tutahakikisha kuna uwajibikaji katika pesa zinazokwenda kwa asasi za kiraia".

Ameongeza kuwa, licha ya Shirika lao kuwa kongwe lakini wamebaini wao wenyewe hawawezi kuwafikia watoto wengi zaidi hasa walioko vijijini, ndio maana wameamua kubadili mitazamo yao ya kisera, pia wamebadilisha hadi mifumo yao ya ndani, wanawajengea uwezo asasi hizo, kwenye mifumo yao ya kitaasisi wakafanye kazi nzuri ili kuhakikisha hakuna mtoto ambae anaachwa nyuma


Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...