WAZIRI MCHENGERWA AMPA TANO KUMBILAMOTO
Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI) Dkt Mohamed Mchengerwa, amemtabiriwa mambo makubwa Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti kwa utendaji bora wa kazi katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Waziri Dkt Mohamed Mchengerwa amesema hayo wakati wa kuzindua mradi wa Serikali wa ujenzi wa soko la nyama choma la lililopewa jina la KUMBILAMOTO mradi huo uliopo machinjio ya Vingunguti wilayani Ilala.
"Nawapongeza Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam mmepata Meya bora Omary Kumbilamoto, mchapa kazi na anafanya kazi kwa weledi za Serikali anajua kazi yake isingekuwa katiba ya chama cha Mapinduzi Meya Omary Kumbilamoto anapita bila kupingwa na Jimbo lingegawanywa angepewa jimbo moja "amessema Dkt Mchengerwa.
Amesema kuwa, kutokana na utendaji kazi wa Meya Kumbilamoto ni vyema madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kumpa ushirikian katika kumsaidi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na kusimamia miradi ya maendeleo vizuri ya Halmashauri.
Wakati huohuo alitoa agizo sheria ibadilishwe Naibu Meya wa Halmashauri achaguliwe kila baada miaka mitano kuanzia sasa sio mwaka mmoja ili kuondoa migogoro ndani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Hata hivyo, amemwagiza Katibu Mkuu TAMISEMI kuwasilisha kanuni haraka Bungeni ili aweze kusaini kurekebisha kabla Bunge la Jamhuri ya Muungano kuvunjwa ili iweze kutumika haraka .
Kwa upande mwingine alimwagia sifa Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya anafanya kazi kubwa katika Wakurugenzi 184 nchini Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam ameshika namba moja anafanya kazi kubwa ya kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kukusanya mapato mengi na kuvunja rekodi.
Akizungumzia suala la amani ya nchi alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuwakamata wote wanaovuruga anani ya nchi yetu kwani katika suala la amani uwezi kuzungumza ukajificha tuilinde amani kwa nguvu zote kwani inapotokea machafuko uwezi kuangalia mzee au kijana.
Kwa upande wake Meya Kumbilamoto, amesema dhumuni la kujenga mradi huo wa nyama choma wafanyabishara waliandamana nyumbani kwake ambapo awali kulienea uvumi eneo hilo la Serikali limeuzwa ambapo taarifa sio za kweli leo mradi wa Serikali umekamilika uliogharimu shilingi bilioni 729.6 fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Meya Kumbilamoto amesema katika mradi huo wa ujenzi wa jengo la soko la nyama choma la Kumbilamoto watafunga TV kubwa za kisasa kwa ajili ya Wananchi waweze kufatilia matukio mbali mbali ikiwemo taarifa ya habari.
Akizungumzia maendeleo ya Serikali kata ya Vingunguti ameweza pia kusimamia DAWASA wananchi wanapata maji safi na salama, sekta ya elimu NMB na Serikali ya Dkt.Samia imeweza kuleta madawati ya kutosha wanafunzi wanakalia madawati na shilingi milioni 700 Rais ameleta kwa ajili ya sekta ya elimu pia
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya ,alisema katika soko hilo la nyama choma Vingunguti kutakuwa na huduma za kifedha ambapo alimpongeza Meya kwa kuizinisha mradi huo wa maendeleo Halmashauri hiyo itasimamia kuwawezesha wajasiriamali wadogo kukuza uchumi wa nchi yetu .
Comments
Post a Comment