DKT MPANGO ATEMBELEA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA UZALISHAJI VIFAA TIBA NCHINI ITALIA





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametembelea Kampuni ya Kimataifa ya Uzalishaji Vifaa Tiba ya Health 3000 iliyopo Roma nchini Italia leo tarehe 23 Juni 2025.

Makamu wa Rais amefanya mazungumzo na viongozi wa kampuni hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Maurizio Flammini pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bi.Eleonora Flammini. Mazungumzo hayo yamelenga ushirikiano baina ya Tanzania na Kampuni ya Health 3000 hususani katika matibabu kwa njia ya mtandao (Telemedicine).

Kampuni hiyo ni moja ya Makampuni yaliyo chini ya mwamvuli wa FG Group ambayo imejikita katika kutoa huduma za afya hususani uzalishaji wa vifaa tiba kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Makamu wa Rais yupo nchini Italia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Ubia wa Maendeleo kati ya Afrika na Serikali ya Italia (Mattei Plan) pamoja na mikutano mbalimbali ya uwili.

Comments

Popular posts from this blog

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU CCM YASHIKA KASI