BAKWATA MWANZA WAWAOMBA WADAU KUCHANGIA UJENZI WA VITUO VYA AFYA


Na Mwandishi wetu, HPMedia, Mwanza

Baraza kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza linawaomba watanzania kutoa michango kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa vituo vya afya saba ambavyo vinajengwa katika halmashauri za mkoa huo.

 Akizungumza na Mwandishi wa Makala hii, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke, amesema kuwa uongozi wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) unaomba watanzania kuendelea kuchangia ujenzi wa vituo vya afya saba  kupitia m.pesa lipa namba, 543032 Bakwata Mwanza jenga hospital au kupitia benk ya CRDB ACC, 0150658188600 Bakwata harambee.

Aidha, amesema kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Oktoba 30, 2022 hadi Desemba 31 mwaka jana uongozi huo umefanikiwa kujenga vituo vya afya saba katika kila wilaya ya mkoa kwa sadaka za waislam na wasiokuwa waislam 


Hata hivyo, amesema uongozi huo chini ya uongozi wake kupitia michango inayotolewa na wadau mbalimbali kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vituo hivyo kupitia kauli mbiu isemayo "Bakwata Mwanza jenga msikiti".



Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI