DCEA YAKAMATA KILO 23.88 ZA MIRUNGI
Na mwandishi wetu, HPMedia, Dar es Salaam
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) January 26 ilifanya Operesheni maalum katika wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam na kukamata Dawa za Kulevya aina ya Mirungi Kilo 23.84.
Aidha, madawa hayo yalikua yamehifadhiwa ndani ya nyumba ya Rhoda Mohamed Salum (48) ambaye ni mkazi wa Lukongo eneo la Wailes Wilayani Temeke akiwa anajiandaa kuzisafirisha kwenda nje ya nchi.
January 27 katika dampo la Kituo cha Polisi Chang'ombe, kiasi hicho cha dawa za kulevya kiliteketezwa chini ya uangalizi wa baadhi ya wadau kutoka taasisi zinazotambulika Kisheria kama ilivyoelekezwa kisheria kwenye kanuni ya 14.
Miongoni mwa watu walioshuhudia tukio hilo nk pamoja na mwakilishi wa Kamishna wa mamlaka ya Kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya, Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Temeke, Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Polisi, Mwakilishi wa Mkemia Mkuu wa Serikali na Mwakilishi kutoka ya mashtaka nchini.
Aidha, uteketezaji huo ulifanyika kuendana na matakwa ya kifungu cha 36(1) cha sheria ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya ambacho kinaruhusu uteketezwaji wa baadhi ya dawa za kulevya kwa kuzingatia hali ya hatari ya dawa hizo,
Kuharibika kwake, athari za mazingira, ufinyu wa mahali maalum pa kuhifadhia au kwa kuzingatia masuala mengine yanayofanana nayo kwa kuwa mirungi hiyo ilikuwa mibichi, kulikuwepo mkubwa wa kuharibika na kupoteza uhalisia wake hivyo ilikuwa muhimu kuteketezwa kwa dawa hizo
Upelelezi wa shauri hili bado unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani
Comments
Post a Comment