JAMAL BABU - TUTAWAJIBU WAPINZANI KWA HOJA

 

Na Mwandishi wetu, HPMedia, Mwanza 

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi CCM yanayotarajiwa kufanyika Feb 5, mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa mkoa wa Mwanza  (Mnec) Jamal Babu amesema wapo tayari kuwajibu wapinzani kwa hoja juu ya miradi inayotekelezwa na Rais Dkt.Samia 

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Mwanza wakati aposhiriki zoezi la kupanda miti katika shule ya sekondari Buzuruga ikiwa ni kuelekea kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa chama hicho ambapo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya miradi mikubwa ya maendeleo hivyo watawajibu wapinzani wanaobeza utendaji kazi wa Rais Dkt Samia.

"Mwenyekiti wa Chama chetu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameruhusu mikutano ya hadhara sisi kama chama tuko tayari tutaenda kuwajibu wapinzani kwa hoja kutokana na miradi inayotekelezwa na mwenyekiti wa chama chetu, Dkt Samia"amesema Babu.

Diwani wa kata ya Buzuruga na naibu meya wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza Manusura Sadiki amempongeza Rais Dkt. Samia Suruhu Hassan pamoja na mbunge wa Jimbo la Ilemela Angelina Mabula kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Buzuruga

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI