JESHI LA POLISI LAPOKEA MSAADA WA COMPUTER



Na Mwandishi wetu, HPMedia,Dar es Salaam 

Jeshi la Polisi limepokea msaada wa kompyuta mpya 20 zenye thamani ya shilingi milioni 30 kutoka Benki ya CRDB leo tarehe 17.02.2023. Makabidhiano ya kompyuta hizo yamefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya CRDB jijini Dar es Salaam.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati wa makabidhiano hayo, Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu, Kamishna Suzan Kaganda ameshukuru kwa msaada huo kwani umekuja katika kipindi ambacho Jeshi la Polisi lipo katika maboresho ya mifumo yake ya kiutendaji. Amesema kompyuta hizo zitakuwa chachu ya mabadiliko hayo hasa katika kusimamia haki jinai.

Aidha Kamishna Kaganda ameongeza kwa kusema kuwa kompyuta hizo zitatumika katika vituoni vya Polisi katika kurahisisha mawasiliano kati ya vituo na makao makuu ya Jeshi la Polisi na kutunza kumbukumbu ili kuondokana na mfumo wa makaratasi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CRDB Tuliesa Mwambapa amesema kwamba msaada huo ni katika kuboresha mahusiano ya Benki ya CRDB na Jeshi la Polisi Tanzania. Ameongeza kwa kusema wametoa kompyuta hizo ili kuchangia katika jitihada za serikali za kuleta mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI