NAIBU WAZIRI MASANJA ABARIKI JIJI LA MWANZA KUWA KITOVU CHA UTALII
Na mwandishi wetu ,HPMedia, Mwanza
NAIBU Waziri wa Mali asili na utalii Marry Masamja amebariki jiji la Mwanza kuwa kitovu cha utalii kutokana na ujenzi wa reli, stendi ya Nyegezi na Nyamhongolo pamoja na kiwanja cha Ndege.
Kauli hiyo ameitoa jiji Mwanza wakati alipokua katika mkutano ambapo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan a a mipango mikubwa na jiji hilo kutokana na miradi mbalimbali inayoendelea.
Aidha, amesema, Mwanza Itakuwa ni jiji namba moja inayotambua uwekezaji unaotokana na sekta ya utalii faida ya utalii ni pamoja na kuongeza mnyororo wa thamani mgeni anapokuja Mwanza anapofikia airpot utauza Samaki, machungwa, chakula mgeni atasafiri atalala mwenye hoteli atafaidika .
"Serikali ya awamu ya sita imejipanga kukuza sekta ya utalii ndio maana imeweka mipango mingi, hivyo kila mmoja wetu awajibike tusimuangushe Rasi wetu, ana mipango mikubwa ya kuifanya Mwanza kuwa ni kitovu cha utalii" amesema Naibu Waziri Marry.
Comments
Post a Comment