RAIS DKT SAMIA AOMBOLEZA VIFO VYA WATU 17
Na mwandishi wetu, HPMedia, Mtandaoni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii amesikitishwa na ajali ya gari iliyosababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 12 huko Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.
Katika taarifa aliyoitoa leo Febr 4,2023 kupitia taarifa fupi aliyoitoa katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii amesikitishwa n vifo vya watu 17 walifariki jana saa 4:30 usiku eneo la magila Gereza, Wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga.
"Nawapa pole wafiwa na wote walioguswa na vifo hivi. Nawaombea ndugu zetu hawa wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka,"amesisitiza Rais Dkt.Samia
Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba leo imeeleza kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili na kusababisha vifo vya watu 17 na Majeruhi 12.
Ajali hiyo imetokea usiku katika eneo la Magira Gereza Kata ya Magira Gereza Tarafa ya Mombo wilayani Korogwe, barabara ya Segera - Buiko.
"Ajali hii imesababisha vifo 17 na majeruhi 12 ambao majina yao wote hayajafahamika, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali yetu ya Wilaya ya Korogwe na majeruhi 10 wamehamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo na majeruhi wawili wamebaki Hospitali ya Korogwe kwa matibabu.
“Ajali hii imehusisha gari aina ya Mitsubishi Fuso na Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu na abiria 26 ikitokea Dar kwenda Moshi kwenye mazishi” imeeleza taarifa hiyo.
Comments
Post a Comment