UVUVI SIO AJENDA YA KISIASA - KADABI
Na Mwandishi wetu, HPMedia, Mwanza
Chama cha Wavuvi Tanzania ( TAFU ) kimewaomba wanasiasa wote nchini kuwasaidia kuelimisha baadhi ya wavuvi , maafisa uvuvi, watendaji wa vijiji, wenyeviti wa serikali na wengineo wote kuacha kujihusisha na uvuvi haramu na badala yake wawalinde samaki kama zinavyolindwa rasiliamali nyengine.
Akizungumza na Mwandishi wa Makala hii kwa njia ya Simu kufuatia hali ya uvuvi haramu, mkoani humo, Mwenyekiti wa Chama wa wavuvi mkoa wa Mwanza (TAFU) Bakari Kadabi amesema ni heri wanasiasa kutoa elimu juu ya watu kuacha uvuvi haramu na watambue umuhimu wa kulinda raslimali za nchi kwa faida ya Watanzania wote.
"Hatuwezi kuepuka siasa na maisha yetu lakini tunaofika kwenye masuala ya kitaalamu wanasiasa watimize wajibu wao kwa kushauri tu, sisi kama wavuvi atuwezi kukubali ziwa Victoria ligeuke kuwa ajenda za uchaguzi mkuu wa Serikali katika majukwaa ya kisiasa" amesema Kabadi
Aidha, amewataka wanasiasa kujiepusha kufanya suala la uvuvi kuwa suala la kisiasa kutokana na baadhi ya wanasiasa kuanza kutoa lugha ambazo zinaweza kuchochea kufanya uvuvi ambao unaweza kuleta madhara ndani ya ziwa Victoria ikewemo uvuvi haramu.
"Tunaiomba Serikali ihakikishe samaki analindwa kama wanavyolindwa wanyama pori katika hifadhi za taifa na inasikitisha kuona maliasili zote zinalindwa kwa kutumia nguvu kubwa sana kuliko maliasili ya uvuvi," amesema Kadabi.
Hata hivyo, amesema wamekuwa msitari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia suala zima la kulinda rasilmali ya samaki ndani ya ziwa Victoria kutokana na uwepo wa kushamiri kwa vitendo vya uvuvi haramu katika ziwa hilo.
Comments
Post a Comment