SERIKALI YAJA NA MPANGO MADHUBUTI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKAZAJI SEKTA YA MADINI

 


Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar 

Waziri wa Madini Dkt Doto Biteko amesema Serikali imerahisisha mazingira ya kikodi kwa wachimbaji wa madini ili kuondoa utiritimba wa kodi na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika kutimiza majukumu yao ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki na bora zaidi.

Kauli hiyo ameitoa jijini  Dar es Salaam wakati akifungua kikao cha wadau wa madini  cha kujadili maendeleo, changamoto na kero na inazozikabili kampuni kubwa za kati zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini katika migodi mbalimbali hapa nchini. 

Aidha amesema Serikali itahakikisha inaweka mipango thabiti ya kutatua  baadhi ya changamoto zilizopo kwenye Sekta ya Madini ikiwemo kuweka  miundombinu rafiki ili kusaidia wawekezaji wanaongeza tija uzalishaji wa madini nchini na Pato la Taifa kukua .

"Mara nyingi huwa tunakutana na wachimbaji wa madini wadogo kuskiliza kero zao lakini leo tupo na wachimbaji wakubwa tujadili kwa pamoja changamoto zao na tuzipatie ufumbuzi, huku tukijiandaa na mkutano mkuu wa kisekta wa mwaka utakaofanyika Oktoba mwaka huu"amesema Waziri Dkt Biteko.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Philibart Rweyemamu amesema kupitia chama anachokiongoza wamejipanga kushirikiana na Serikali ili kuondoa changamoto na kutoa na kupata suluhisho la kudumu  hatimaye kufikia lengo la kuchangia asilimia 10 kwenye Pato la Taifa ifikapo 2025 kama ilivyo azma ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

"Kikao cha namna hii kitakuwa kinafanyika kila robo mwaka ili kutoa taarifa kwa Serikali juu ya maendeleo ya shughuli zetu, kuueleza umma nini kinachofanyika pamoja na kuishauri Serikali kitu gani tunafikiri kifanyike ili kurahisisha utendaji wa Sekta ya Madini," amesema Mhandisi Rweyemamu.


Naye, Waziri wa Madini Maji, Nishati na Madini kutoka Zanzibar, Staibu Hassan ameipongeza Wizara ya Madini kwa hatua kubwa kwani wizara hiyo imekuwa mwalimu wa mataifa mengi kujifunza usimamizi bora wa shughuli za biashara na uchimbaji madini.

Katika kikao hicho Kampuni tano za uchimbaji mkubwa wa madini zimetoa taarifa za utekelezaji wa miradi inayotekelezwa ikiwemo Kampuni ya Nyati Corporation, Sotta Mining, Tembo Nickel Corporation, Twiga Minerals na Faru Graphite Limited.



Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI