WATANZANIA WATOLEWA HOFU KUJIUNGA VYUO VYA NJE YA NCHI
Na Mwandishi wetu HPMedia, Dar
Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Education Link Abdulmak Mollel amewatoa hofu wazazi wanaoogopa kuwapeleka watoto wao kusoma nje ya nchi kwa kuhofia gharama kubwa za ada na kujikimu wanapokuwa masomoni.
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakat alipotembelewa katika banda lao na Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ambapo amesema vipo vyuo vya nje vinavyofundisha kwa gharama nafuu zaidi.
Amesema kuwa, kampuni yao inasimamia vyuo bora 14 ambavyo vinayoa elimu yenye ubora na kiwango na inayokidhi soko la dunia hivyo ni vyema wazazi na walezi kuwapelekq watoto wao kuunganishiwa kusoma nje ya nchi kw hana shaka na elimu ya juu inayotolewa na vyuo ambao wameingia navyo ubia.
Amesema kampuni hiyo inayojihusisha uwakala wa kupeleka wanafunzi kusoma nje ya nchi ina vyuo bora 14 vya gharama nafuu ikiwemo katika nchi za Uturuki, India, Canada na Malawi ambapo amesema wanatamani waone sylabus za kitanzania zikifundishwa katika vyuo hivyo.
Aidha amesema India ni miongoni mwa nchi zinazotoa elimu bora kupitia vyuo vyake lakini hufundisha masomo ya uhandisi kwa gharama nafuu, mwanafunzi anayepata bahati ya kujiunga na vyuo hivyo hutumia dola 510 kwa ajili ya chakula mwaka mzima huku ada ikiwa ni dola 1500 ambayo mtanzania anaweza kumgharamia mwanafunzi kwa kulipa kidogo kidogo mpaka mtoto wake atakapohitimu mafunzo yake.
"Tunatamani mafunzo ya kozi za uhandisi wanafunzi waweze kwenda kusoma nje ya nchi ili wapate teknolojia mpya hivyo tunaweza kuwaomba wazazi wawalete watoto wao hapa glaballink ili tuwafanyie udahili na wasiogope kiingereza kwani ni sawa na kile walichofundishwa mashuleni hapa nchini"amesema Abdulmalik.
Comments
Post a Comment