TMA YATOA TAAHADHARI UWEPO WA JOTO

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inapenda kutoa taarifa ya tathmini ya hali ya joto na mwenendo wake katika maeneo mbalimbali nchini. 

Ongezeko la joto nchini husababishwa na kusogea kwa jua la utosi sambamba na upungufu wa mvua unaojitokeza katika maeneo mbalimbali. Kwa kawaida vipindi vya jua la utosi nchini hufikia kilele mwishoni mwa mwezi Novemba wakati jua la utosi likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena mwezi Februari wakati jua la utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa). 

Aidha, wastani wa ongezeko la joto la dunia katika mwaka wa 2023 ulifikia nyuzi joto 1.40C na ulivunja rekodi na kuwa ni mwaka wenye joto zaidi katika historia ya dunia, ukichagizwa na uwepo wa El Niño na mabadiliko ya tabianchi.

 Kwa upande wa Tanzania, tathmini zinaonesha pia wastani wa ongezeko la joto kwa mwaka 2023 ulikuwa nyuzi joto 1.00C kwa upande wa Tanzania na pia kuufanya mwaka 2023 kuvunja rekodi na kuwa mwaka

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI