MFUMO HAKIJINAI BADO KIZUNGUMKUTI WATU KUPATA HAKI ZAO
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar
Mkurugenzi wa Taasisi ya Everlastins Legal Aid Fiundation (ELAF) Dkt Khamis Massoud amesema Mfumo wa haki jinai una mapungufu mengi sana ikiwemo haki ya dhamana na namna uchunguzi unavofanyika kudumu kwa muda mrefu mpaka mtu anakata tamaa kudai haki yake.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwenye mahojiano maalum ya kutaka kujua namna mfumo huo unavyofanya kazi ambapo amesema kumekua na ukirikimba mkubwa sana kwenye kupata dhamana kwa mtuhumiwa.
Amesema kuwa, unaweza ukakutana na mtu anakwambia ndugu yake amewekwa mahabusu namna ya kufuatilia dhamana unamuliza amewekwa kwa kosa gani anakupa RB no unaona imeandikwa jalada la uchunguzi, hiyo sio sawa kwa sababu tumeshazoea kumuona mtu akiwekwa ndani kwa kosa la wizi, ubakaji ama ulawiti ila jalada la uchunguzi inakuwa hakuna tuhuma iliyowekwa wazi.
Ameongeza kuwa,"Mfano mtu anaweza akawa amepoteza simu ya laki 3 akaripoti Polis anakwambia anaweza akatumia zaidi ya mill moja na muda mwengine anaefatilia kesi yame anaweza akasema yupo busy na muda mwengine hana nauli, hata wale watu wa mawasiliano wamekua wakilalamikiwa sana kutokua na uharaka wa kufuatia matukio" amesema Dkt Massoud.
Amesema kuwa, kuna jambo la kujifunza kuhusiana na dhamana yapo makosa ambayo unaweza ukajidhamini mwenyewe kulingana na aina ya kosa kupitia ID no kitambulisho cha Nida kwa maana kina taarifa zote muhimu za mtuhumiwa unapomwambia alete watumishi wa Serikali ili apate dhamana kama hana inabidi aende akawanunue jambo ambalo si sawa.
Hata hivyo, amesema kuwa, hata kwenye mfumo wa uchunguzi umekua na changamoto kukaa muda mrefu, mfano kesi ya ubakaji inawezekana wale watu waliotakiwa waende wakatoe ushahidi unakuta wameshahama na kuhamia sehemu nyengine, mtuhumiwa anaachiwa huru kwa sababu hakuna mashahidi.
"Vitu vyengine ni rushwa mukhali 'rushwa ya kumuonea mtu aibu' mfano kesi ya kulawiti kwa sababu alietenda kosa lile ni jirani yake anashindwa kutoa ushahidi, akimuhofia sasa hapa elimu kubwa sana inahitajika ili watu waweze kupata haki zao bila kuoneana aibu "
Sambamba na hayo amesema pia sababu nyengine ni migogoro ya ardhi na mali hasa kwenye familia hizi kesi zimeshamiri sana watu kugombeana mali, mfano nyumba au ardhi wakati mwengine unakuta eneo moja limeuzwa zaidi ya mara moja na watendaji wa mitaa wamekua wakishuhudia.
Comments
Post a Comment