ZITTO AWAFUNDA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU, ASHUSHA NONDO NZITO
Na Mwandishi wetu, HabarPlus 24, Dar
KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewataka wanachama wa Chama hicho kukataa kupokea malalamiko ya mtu yoyote anataka kuwaganya huku akiwataka waendelee na mshikamano wao wa kujenga na kukiimarisha chama chao.
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo wakati alipokua akihutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu kupitia kikao maalum ambacho kimehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 119 ambapo kimelenga kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo Katiba ya uchaguzi .
"Mtu yoyote atakaekuja kuwapa malalamiko yoyote yanayoashiria kuleta mtafaruku kwenye chama ama kutaka kutugawanya naomba musikubali na muyapuuze na tuendelee na mshikamano wetu wa kujemga na kukiimarisha chama chetu na kuyafikia malengo yetu tuliojiwekea"amesema Zitto
Amesema kuwa, Chama hicho kimeendelea kujiimarisha kitaasisi kwa kuanzisha taasisi mbili muhimu ambazo zinatekeleza malengo na madhumuni ya chama na kuhakikisha ustawi wa wanachama ambapo taasisi hizo ni Baraza Kivuli la Mawaziri na Shusha Tanga Saccos.
"Baraza kivuli la Mawaziri ambalo lipo chini ya uongozi wa Waziri Mkuu kivuli, Dorothy Semu na Katibu Mkuu Kiongozi Idrissa Kwaweta, hili limelenga kukosoa sera za Serikali iliyopo madarakani na kupendekeza mbadala wa sera, tumeona baadhi ya mapendekezo ambayo tunayatoa serikali wanayafanyia kazi"amesema Zitto.
Aidha, ameongeza kuwa Taasisi ya Shusha Tanga Saccos, ni taasisi ya hiari na ya wanachama wenyewe kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za kimaisha kutokana na mambo ya mikopo yenye riba kubwa maarufu kama Kausha Damu, hivyo kuwepo kwa taasisi hiyo ndani ya chama kutasaidia wananchama wenyewe kuweza kujisaidia katika mambo mambo mbalimbali.
"kutokana na usajili wa wanachama uliofanywa kwenye saccos hii hauna nguvu, hivyo niwasihi wajumbe wa Halmashaur Kuu ya Chama Taifa kwanza nyinyi wenyewe muwe mfano kwa kujiunga ili kuonesha njia ya kuhamasisha wanachama wengine"amesema Zitto.
Aidha amesema kuwa,wamefanikiwa kuchagua uongozi katika majimbo yote 264 nchi kote ambapo majimbo 214 ni ya Tanzania bara na 50 Zanzibar, huku mikoa yote ikichagua viongozi wake jambo ambalo ni ishara ya ukuaji na nguvu ya chama hicho.
Sambamba na hayo, amesema kuna masuala mahususi ambayo yasipochukuliwa hatua yanaweza kusababisha madhara makubwa kwa taifa ikiwa ni pamoja na migogoro ya ardhi na migogoro ya mipaka kati ya hifadhi na vijiji, pamoja na kupanda kwa gharama za maisha.
"Chama chetu kinaendelea kutoa wito kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutimiza wajibu wake huo, kupitia baraza Kivuli la Mawaziri tumekuwa tukitoa majawabu ya hatua zinapopaswa kuchukuliwa, Serikali kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kuongeza tija kwa mkulima"amesema Zitto
Aidha, ameongeza kuwa ACT - Wazalendo walipeleka mapendekezo 10 ya miswada Bungeni ambapo 6 yamechukuliwa kama yalivyo,yamebaki mambo manne hivyo wanajipa moyo kuwa mabadiliko hayo ni hatua muhimu sana katika safari yao ya kudai chaguzi huru na zenye haki na kuacha alama ya kudumu katika nchi kupitia chama chao.
"Miswada ilikua na mambo mengi sana chama chetu kupitia kamati kuu yetu ya chama tulichambua na kupendekeza mambo 10 mahususi ya kuyabeba na kuyawasilisha bungeni, kati ya mambo 10 tuliopendekeza 6 yamechukuliwa kama yalivyo na kuwekwa katika sheria hizo mpya"amesema Zitto.
Comments
Post a Comment