HOSPITAL YA MNAZI MMOJA YAPATA MSAADA
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Media
Waandaji wa mbio za Absa Dar City Marathon kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametoa msaada wa vifaa tiba katika kliniki ya mama ya mama na mtoto katika hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam l3ngo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali kwenye kuboresha huduma za afya.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa The Runners Club, Godfrey Mwangungulu amesema Serikali imekuwa ikifanya juhudi kubwa zaidi za kuhakikisha kwamba zinaboresha huduma za afya hivyo wao kama wadau wameona wawe sehemu ya wamoja wa kusaidia mchakato huo.
"Vifaa hivi tulivyovitoa katika wodi ya wakina mama katika hospitali hii ni kompyuta na vifaa vingine mbalimbali, Rais Samia amefanya juhudi za kuhakikisha vifaa vinakuwepo vya kutosha katika hospitali mbalimbali nchini"amesema Mwangungulu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga amesema tafiti zinaonyesha kuwa wodi hiyo inauhutaji mkubwa wa kompyuta hivyo wanahakikisha wanawapatia kompyuta hizo ili waweze kuwahudumia wakina mama katika wodi hiyo.
Naye, Meneja Masoko na mauzo wa Alliance Life Assurance LTD, Josephine Mfikwa amesema katika juhudi zao za kutoa huduma za maisha, wanamuangalia mlaji hivyo wanaungana na Runners Club katika kuunga mkono uhai wa watanzania
"Tutaendelea kuunga mkono juhudi hizo za Runners Club na kuendelea kuunga mkono afya ya watanzania,hii ni 2024, hivyo 2025 pia tunampango wa kuendelea kuunga mkono juduhi hizi kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema"amesema
Delila Moshi, Daktari Mfawidhi wa Mnazi Mmoja Hospitali, amewashukuru wadau hao kwa kuendelea kuwaunga mkono mara kwa mara, hivyo amewaomba wadau wengine mbalimbali kuendelea kuwaunga mkono pia kwani changamoto bado ziko nyingi katika hospitali hiyo.
Comments
Post a Comment