MANDASI STORE KIMBILIO LA VIJANA "UCHUMI KIGANJANI"SIMU BEI CHEEE
Na Mwandishi wetu, Habari Plus, Dar
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Omar Kumbilamoto amewataka wananchi wa jiji hilo kuchangamkia fursa ya kutumia simu janja zinazopatikana katika maduka ya mandasi yaliopo katika mikoa mbalimbali Tanzania.
Aidha, amewataka wadau mbalimbali wakiwemo maboda boda, watumishi wa umma pamoja watu binafsi wanaokopa simu katika maduka hayo kuwa waaminifu kwa kulipa mikopo yao ili na watu wengine waweze kukopa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua duka kubwa na la kisasa la Simu,vishikwambi na laptop (Mandasi Store) lilipo maeneo ya Banana jijini humo ambapo amesema ni hatua kubwa iliyofanywa na kampuni hiyo huku akipongeza hatua ya kutoa ajira kwa vijana.
"Nimekuwa nikiitwa kufungua maduka mengi ya kuuza simu lakini yamekuwa ya gharama kubwa lakini kwa Mandasi ni tofauti nimekuta simu za bei ya kawaida ambazo kila mmoja ataweza kuzipata na hata kama hana hela taslimu anaweza kukopa na kulipa kidogo kidogo"amesema Mstahiki Meya Kumbilamoto.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mandasi Store Abdillah Mandasi amesema tangu ameanza biashara hiyo ya kuuza na kukopesha simu kampuni hiyo imekua ikifanya vizuri ambapo sasa imefika katika mikoa 10 wakifungua matawi 14 .
Amesema kuwa, wameanza kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini wameshatoa mikopo ya simu zaidi ya elfu 26,000 ambapo wanamaduka 14 ndani ya mikoa 10 Tanzania nzima ambapo kwa jiji la Dar es Salaam wapo maeneo makumbusho, banana, Chanika pamoja na Mlimani City.
Ameongeza kuwa, wametoa ajila kwa vijana wa Kitanzanzia zaidi ya 36 na wameahidi kuendelea kutoa ajila kwa kukuza huduma hiyo kwa kufungua maduka zaidi katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza kuhusu bei amesema kuna simu janja zinazoanzia Tsh 100,000/=., laki mbili hadi milioni tatu ambapo kwa za bei ya juu zaidi mkopaji anatakiwa kuwa mtumishi umma ili kurahishia ufuatiliaji wake.
Nae mtangazaji wa wasafi Diva the boss lady, ambae ni balosi wa Kampuni hiyo amesema wakua wakitoa simu zenye ubora kwa bei rahisi huku masharti yao yakiwa mepesi sana ikiwemo kitambulisho cha nida na pesa ya kianzio kulingana na aina ya simu ambayo mtu anaitaka.
Nae Doto Magari amewapongeza Mandasi store kwa kuwa na huduma za maduka nchini ambapo wanatoa ajila kwa vijana pia wanatoa huduma za kuuza simu na mikopo ambapo inawawezesha watu wakipato cha chini na cha kawaida kupata simu na kulipa kidogo kidogo.
Comments
Post a Comment