WAZIRI MKUU MGENI RASMI KONGAMANO LA JUMIKITA LA MIAKA 3 YA RAIS DKT SAMIA
Na Mwandishi wetu,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la maadhimisho ya miaka mitatu ya Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii (Jumikita) jijini Dar es Salaam.
Aidha, wanatarajia kuwaalika wageni zaidi ya 500 ambapo mada zaidi ya tano (5) zitajadiliwa, hivyo amewaomba wanachama wa Jumikita washiriki kikamilifu kwenye shughuli hii ya kihistoria kwani ni tukio lao.
Akizungumzia na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jumikita Shaban Matwebe amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kujadili miaka mitatu ya Rais Dkt Samia katika uhuru wa habari.
"Pamoja na kuadhimisha miaka mitatu ya Jumikita, tutakuwa tukiadhimisha miaka mitatu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na siku ya uhuru wa Vyombo vya habari Duniani, ambapo kongamano hili litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa"amesema Matebwe.
Amesema kuwa, kongamano hilo litakalofanyika Mei 20, 2024 kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
"Napenda kutumia nafasi hii kuwajulisha kuwa, kwenye kuadhimisha miaka mitatu, Jumikita kwa kushirikiana na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO), tutafanya Kongamano kubwa kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 20/5/2024," amesema Matwebe na kuongeza,
Hata hivyo, Matwebe ametumia fursa hiyo kuwapongeza wanachama wa Jumikita kwa kuendelea kulitumikia Taifa kupitia Uwanja wa Mitandao ya Kijamii.
"Kazi yenu inahitajika mno kwa Taifa letu. Nafasi yetu ni dhahiri. Umuhimu wetu haukwepeki. Ni kwa msingi huo, ninayo furaha kubwa kuwapongeza kwa kufikisha umri wa miaka mitatu ya Jumuiya yetu," amesisitiza Matwebe.
Comments
Post a Comment