BOCO ATUA JKT TANZANIA


Na mwandishi wetu, HabariPlus

Timu ya Mpira wa Miguu ya JKT Tanzania imesajili aliyekua mchezaji wa mpira wa Timu ya Simba Sport Club John Raphael Bocco ambapo atatoa kichapo cha kizalendo kwa timu pinzani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Msemaji wa timu ya JKT Tanzania Masau Bwire amesema usajili huo wanaamini utaiwezesha timu hiyo kutwaa kombe au kishika nafasi nne za kwanza ili iweze kushiriki michuano ya kimataifa.

"Timu yetu ni ya kizalendo inajali wazawa na haina mchezaji wala kiongozi yeyote toka nje ya nchi, tunaimani na vipaji vya watanzania Bocco mliemtazama katika msimu uliopita mliona kazi yake niseme kwamba huku amezaliwa upya, baada ya usajili tu yeye alikuwa wa kwanza kufika kambini tulianza naye na ameonesha nidhamu ya hali ya juu"amesema Bwire.

Wachezaji wengine waliosajili ni kutoka Uhamiaji Zanzibar, Charse ilamfya toka mtibwa, Kipata KMC Denisi Richard,karimu mfaume fikiri toka biashara,Twalipo elisha Jafeti, Hamisi Salum Hamisi-,Kombo Hatibu anaemalizia mafunzo ya kijeshi na TMA ya Arusha Wilson Nangu.

"Tunao wachezaji wengine takribani wawili bado tunaendelea kukamilisha mchakato wa usajili wao kutoka katika timu zao,sisi ni timu ambayo tunapenda kukamilisha taratibu za kuhamisha wachezaji hatupendi mitifuano na mvurugano kwetu maridhiano ndio jambo la msingi"amesema Bwire

JKT Tanzania wanatengeneza uwanja wenye viwango vya kimataifa ambapo utaambatana na VVIP ambao mtazamaji wa mpira akikaa kwenye jukwaa ataburudika na vitu vingi upande mmoja utakuwa na zoo,na upande mwingine bahari utakuwa ni uwanja wa aina yake.

Hata hivyo amebainisha kuwa ifikapo mwezi wa nane uwanja utakuwa umekamilika ambapo wanategemea mashabiki elfu nane 8 hadi elfu kumi 10 watakaa kwa nafasi bila kubughudhiwa wakitazama soka .

Katika hatua nyingine JKT Tanzania imetangaza rasmi Kubadili mfumo wa uongozi katika klabu hiyo pamoja na klabu ya JKT Queens na ambapo zitakuwa na uongozi wa pamoja tofauti na hapo awali ambapo kila klabu ilijitegemea.

Msemaji wa timu ya JKT Tanzania Masau Bwire Amesema wamefanya mabadiliko mbalimbali ikiwemo katika nafasi za uongozi. ikiwemo :- Mlezi wa timu zote mbili ni Hassani Rashidi Mabeyo, Mwenyekiti wa Bodi ni Kanali Jophrey Roidi mvula, Wajumbe wa bodi ni Luteni Kanali Mkuu,Luten Kanali Salumu mangapi, Meja Salumu Chamsam,Mtendaji mkuu wa JKT Tanzania ni Jemedari Saidy Kazumali,

Masau ameongeza kuwa Utaratibu umebadilika katika uendeshaji wa timu hizo katika nafasi hizo ambapo nafasi nyingine zimeongezwa na nyingine zimepunguzwa ambapo kumeongezeka nafasi ya waratibu wa timu ambapo watakuwa na wajibu wa kuripoti kwa Mkurugenzi mkuu.

Mratibu upande wa JKT Tanzania ni Stan Joseph Chahe, na kwa upande wa JKT Queens ni Meja Esta Rioba.

Pia kuna idara mbalimbali ikiwemo Mkurugenzi wa ufundi ambapo itasimamiwa na Mwalimu Hamadi ally, kurugenzi ya mashindano, fedha Meja innocent Ndunguru,sheria Captein Immaculate Ediga Mapunda,masoko Sekeratusi Mengela Lubinga na idara ya habari na mawasiliano Masau Bwire.

Aidha amebainisha kuwa Watakuwa na siku ya wazalendo ambapo itafanyika kwa upekee wake hivyo wapenzi wa burudani wasikose.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI