NCCR-MAGEUZI WAMKALIA KOONI MBATIA, WADAI AMEPORA MALI ZA CHAMA

 

Na Mwandishi wetu, HabariPlus

Chama cha NCCR-Mageuzi kimeishutumu Ofisi ya RCO wa Mkoa wa kinondoni kwa kumlinda aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia kwa kupora mali za Chama na kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kny Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Faustin Sungura amedai kuwa awali Ofisi ya RCO wa Mkoa wa Kinondoni walizuia lisifunguliwe jalada kuhusu upelelezi wa aliyekua Mwenyekiti wa Chama hicho James Mbatia kutokana na kupora mali za Chama.

Amesema kuwa, hatua ya chama hicho kumfungulia jalada la upelelezi Mbatia ni miongoni mwa hatua walizozichukua dhidi yake baada ya mkutano mkuu wa chama hicho kumsimamisha na kumvua uongozi na uanachama kwa utovu wa nidhamu.

"Mkutano mkuu uliofanyika Sept 24,2022 jijini Dodoma mbali na utovu wa nidhamu pia amepora baadhi ya mali za chama ikiwa ni pamoja na nyumba 2 zilizopo katika eneo la Bunju B katika wilaya ya kinondoni na kuziuza kwa Tino kwa shill mill 67,000,000"amesema Sungura.

Ameongeza "alipora shamba lenye ukubwa wa hekari 56 katika kijiji cha kirimo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani na kujipatia kiasi cha shill mill 164,500,000 kwa kuuza hekari 47 kati ya 56 zilizpo katika eneo hilo, pamoja na mambo mengine mkutano huo uliuagiza uongozi wa chama kumchukulia hatua za kisheria"

Amesema kuwa, chama kilikusanya vielelezo na ushahidi wote wa umiliki wa nyumba na shamba ambapo March 28 hadi 29 mwaka 2024 chama hicho kilikwenda kufungua jalada dhidi yake juu ya udanganyifu alioufanya lakini RCO mkoa wa kinondoni aliwazuia OC - CID wa mbweni kufungua jalada hilo.

"Alidai kuwa pamoja na ofisi ya RCO wa kinondoni kumlinda James Mbatia ili asifikishwe mahakamani lakini bado Chama chetu kina imani na ofisi ya DPP wa mkoa wa kinondoni,hivyo tutakwenda kufungua jalada kwani CAG amethibitisha kuwa hakua na mali".

Hata hivyo, chama hiko kimewataka wavamizi wote wanaoishi au kufanya biashara kwenye nyumba hizo wawe wameshaondoka kabla ya Julai 30 mwaka huu ili kupisha ukarabati mkubwa unaotarajiwa kuanza Agost 1,2024 ambapo wamepeleka notice ya kuwataka wahame mara moja.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI