TUZO ZA SWAHILI FESTIVAL KUTOLEWA RWANDA

 Na Mwandishi wetu,

Kampuni ya A2V Television Studio, imeandaa tuzo za filamu za kiswahili Afrika, lengo kuu ni kukuza kiswahili kupitia vipindi vya television, filamu katika  nchi za ukanda wa Afrika Mashariki hasa zile zisizozungumza lugha ya Kiswahili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Baraka Chigele, Mkurugenzi wa kampuni ya A2V Television Studio amesema kuwa, mchakato mzima wa ukuzaji kiswahili, filamu na utoaji wa tuzo utasimamiwa na Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo kupitia Baraza la Kiswahili la taifa na bodi ya filamu Tanzania.

Amesema kuwa, tamasha limepewa jina la International Film Festival Afrika Award 2024,2025 ambpo uzinduzi wake ulifanyika Julai 7, 2024 jijini Dar es Salaam na kutamatika kwa mashindano ni Novembe 28, 2025 Kigali nchini Rwanda, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Bi Jannette Kagame.

"Tamasha litafanyika nchini Rwanda huku likihusisha nchi zote za Afrika ambazo zipo tayari kuleta filamu zao  za kiswahili kuingia kwenye mashindano, lakini pia hata zile zilizopo nje ya Afrika zinaruhusiwa ili mladi tu ziwe zimetumia lughaya Kiswahili hata kwaudogo"amesema Chigele 

Ameongeza kuwa, mpaka sasa nchi 16 kutoka Afrika zimekubali kushiriki mashindano hayo, na nchi 2 kutoka nje ya Afrika ambazo ni Canada na Ujerumani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa mashindano hayo, Jamal Mbaga, amesema sababu ya kuanzishwa mashindano hayo, kiswahili kwa sasa ni lugha ya kimataifa hivyo kuna haja ya kukitanua zaidi. 

"Katika lugha 10 zinazokua kwa kasi hapa Afrika lugha ya Kiswahili inaongoza hivyo kuna kila haja ya kukieneza zaidi na sisi tunataka kukieneza kupitia filamu za kiswahili kutoka Tanzania" amesema Jamal

Ameongezea kusema kwamba ni muda sasa wasanii wa filamu kutoka Tanzania kutengeneza kazi nzuri na zenye ubora ili kushindanishwa na wasanii wengine wa filamu Duniani kote.

Aidha, wasanii wa filamu kutoka Tanzania wametakiwa kupelekea kazi zao kwenye mashindano hayo bila ya kuogopa kwani hii ni mara ya kwanza kuanzishwa mashindano hayo, huku ikielezwa kwamba majaji watakaotoa maamuzi hawatakua na upendeleo wowote. 

Hidaya Njaidi ambaye ni barozi wa mashindano hayo  akisisitiza wasanii wa kuigiza waende shule wasome juu ya kile wanachokifanya.

"Kwani vyuo mbalimbali vipo tayari kupokea wasanii wa maigizo ili iwasaidie kuandaa kazi zenu kwa mashindano ya kimataifa" amesema Hidaya 

 Aidha, wasanii wa maigizo wametakiwa kutumia vizuri hii nafasi kwani ni miongoni mwa sababu itakayosaidia kupelekea kazi zao kimataifa ambapo ni miongoni mwao.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI