WAUMINI WA KANISA LA KIBOKO YA WACHAWI WAILILIA SERIKALI, WAJIPANGA KUKATA RUFAA
Waumini wa kanisa la CAC (kiboko ya Wachawi) wameiomba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kulifungulia kanisa hilo ili waumini hao waendelee kupata huduma ya kiroho kama ilivyokua hapo awali.
Aidha, wameitaka ofisi ya msajili kuweka wazi ni changamoto zipi zilipolekea kufungiwa kwa kanisa hilo, ukiachana na iliyoelezwa kuwatoza fedha waumini wake wakati wa kutoa huduma.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Nabii na Mchungaji wa Taifa Komando Daudi Mashimo amesema kuwa hata kama amekosea alipaswa kupewa onyo na sio kufungiwa moja kwa moja.
Amesema kuwa, Mchungaji huyo anatoa huduma kama wanazotoa wangine kama kuna utofauti wowote umeonekana basi ni vyema wakaka nae wakamrekebisha maisha mengine yakaendelea.
"kuna watu mbalimbali hapa wanakuja kufuata huduma kutoka mikoani hadi nje ya nchi, kufungwa kwa kanisa hili limewaathiri waumini hawa pamoja mambo mengine kundi kubwa la boda boda ambao walikua wanategemea abiria kuwaleta hapa"amesema Mchungaji mashimo.
Hata hivyo, amesema wanajipanga kwenda kukata rufaa kutokana na kufungiwa kwa kanisa la kiboko ya wachawi.
Kwa upande wake, Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo, Athanas Msumari amesema suala la mchungaji huyo kuweka kiwango cha shill laki 5 kwa ajili ya waumini kwenda kumuona, hizo pesa zinatumika kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi na huduma mbalimbali.
Pasta Anna Sunza amesema kuwa amehangaika na magonjwa muda mrefu hospitalin bila kupona lakini alipofika kwa mchungaji Dominic amepona ugonjwa wa moyo ambao ulikua unamsumbua muda mrefu.
"Kufungiwa kwa kanisa hili kumetuathiri sana, watu wamekua wakizungumza maneno mengi lakini si kweli mchungaji wetu si tapeli kama watu wanavyoongea, anafanya huduma kama ambavyo wanatoa watungaji wengine"amesema
Baadhi ya waumini hao wamesema kuwa biashara zimekua zikizorota sana tangu kufungwa kwa kanisa hilo licha ya kutoa huduma lakini pia ajira za watu wengi zimepotea ikiwemo mama ntilie, bodaboda na wauzaji wa maduka pembeni mwa kanisa hilo.
Comments
Post a Comment