DART NA UDART ZATAKIWA KULETA WAWEKEZAJI WAZAWA MABASI YA MWENDOKASI




Na Mwandishi wetu,Dar

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa (Mb) ameutaka wakala wa mabasi yaendayo haraka (Dart) na watoa huduma za usafirishaji abiria katika jiji la Dar es Salaam na Pwani (Udart) kukaa pamoja kuleta kampuni za watanzania kuwekeza katika miradi wa mwendokasi.



Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizundua mfumo wa kununulia tiketi kupitia kadi janja na mageti janja kwa akili ya mabasi yaendayo haraka ambapo amesema katika jijini hilo kuna uhaba wa mabasi yaendayo haraka 670 hivyo kutumia wawekezaji wazawa kutasaidia kuondoa kwa changamoto hiyo.

"Nikiri kusema tuna changamoto ya uhaba mabasi, naagiza hadi kufikia disemba mabasi 670 yawe yamefika, bado kuna miradi inaendelea ni vyema kuwaleta wawekezaji wazawa kuja kuwekeza kwani uwezo wanao ili kumaliza changamoto ya usafiri jijini Dar es Salaam, kuliko kukaa kuwasubiri wawekezaji kutoka nje ya nchi"amesema Waziri Mchengerwa.



Amesema kuwa, wazabuni wa kitanzania wanauwezo makubwa sana wa kutoa huduma za usafirishaji kwani kuna kampuni inamiliki mabasi ya kwenda mkoani zaidi ya 20, ambapo inahudumia mikoa yote, hivyo ni vyema kuwaleta wazawa kukabiliana na changamoto hii.

Aidha, amesema kutumika kwa kadi hizo ni kurahisisha usafiri pamoja na utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kadi hizo zitasaidia kuoakoa muda kwa abiria na kuondoa changamoto ya malalamiko ya watu kukaa muda mrefu kwenye jukata tiketi.



Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Dart Athuman Kihamia amesema kadi hizo ni za kisasa, zinaubora sana ambazo ni tofauti na zile zinazotumika uwanja wa Taifa, hivyo. wameanza kwa awamu ya kwanza lakini watazitumia kwa awamu zote sita kwani  zinavitu vingi.

Aidha, amesema kuwa kadi hizo ni za kukusanyia nauli ambapo wataachana na mfumo wa kutumia makaratasi kwani zinachafua mazingira, pamoja na mambo mengine kadi hizo ni nzuri sana ambazo ziondoa malalamiko ya abiria kuhusu kudai chenji zao.

"Pia mfumo unakwenda kuondoa foleni iliyokuepo Kwa abiria wakti wa kukata tiketi na itafanikisha abiria kuingia kwa haraka na abiria kuanza safari, ambapo mfumo huu utaendana sambamba na upatikanaji wa mabasi na tutapata mafanikio makubwa"

Naye, Mwenyekiti wa kamati ya Bunge amesema kuwa, uwepo kadi hizo kutaendana sambamba na kupunguza uhaba wa mabasi, huku amewapongeza Dart kwa kutekeleza agizo la Bunge juu ya kukusanyia nauli kwa njia kieletroniki.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU HAPA MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" , UPEPO KUVUMA KWA KASI YA KILOMITA 130 KWA SAA

NHIF YAFANYA MABORESHO YA KITITA CHA HUDUMA ZA MATIBABU, YAENDELEA KUPOKEA MAONI