"BADO MWITIKIO WA KUJIANDIKISHA NI MDOGO" DOYO
Katibu Mkuu wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Doyo Hassan Doyo amesikitishwa na mwitikio mdogo wa wananchi kwenda kujindikisha katika daftari la mpiga kura.
Kauli hiyo ameitoa jijini Tanga wakati alipokwenda kujiandikisha kwenye daftari la makazi katika kata ya Mabada, mtaa wa Kwedigongo, Handeni Tanga, katika shule ya msingi Kwediziwa, ambapo amesema mpaka sasa idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza kujiandikisha katika daftari mkazi,
Aidha, ametoa wito kwa TAMISEMI kuongeza juhudi za uhamasishaji ili wananchi wengi waweze kujitokeza na kupata nafasi ya kujiandikisha katika daftari hilo, na hatimaye kupata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji.
Pia Katibu huyo amezungumzia umbali wa vituo vya kujiandikisha, huku akihimiza TAMISEMI kuongeza vituo ili kupunguza umbali wa kwenda kujiandikisha jambo ambalo litawarahisishia wananchi.
"Kati ya kituo na kituo, inachukua kilomita 1, kuna haja ya TAMISEMI kuweka vituo karibu zaidi ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kumpa mtu sababu ya kutokwenda kujiandikisha" alisisitiza Mhe. Doyo. "Hii inaweza kuwa sababu moja wapo ya watu kushindwa kujiandikisha."
Comments
Post a Comment