KAPINGA AHAMASISHA WANANCHI MBINGA KUJISAJILI KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA


Na Mwandishi wetu 

Naibu Waziri Nishati na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Judith Kapinga amewahamasisha wananchi katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika zoezi  la kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili waweze kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo. 

Mhe. Kapinga amesema hayo hivi karibuni wakati akifungua Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi, Watendaji na Wadau wa Wilaya ya Mbinga.

"Ni muhimu kila mmoja wetu akashiriki zoezi la kujiandikisha,  sio kujiandikisha wewe tu bali kuhamasisha na wengine kwenye eneo lako waweze kujiandikisha." Ameeleza Kapinga

Amesema ili wananchi waweze kuweka viongozi imara watakaofaa kwenye jamii, ni lazima kuwe na watu wengi wa kuwapigia kura, hivyo ni vyema wananchi wakahamasishana ili kwenda kwa wingi  kujisajili kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi kuchagua viongozi  watakaowatumikia  kwa weledi na kutatua changamoto mbalimbali pale zinapojitokeza.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI