KUMBILAMOTO AWATAKA WAZAZI KUHUDHURIA VIKAO VYA SHULE
Wazazi na walezi wametakiwa kushiriki katika vikao vya shule vinavyoitishwa na walimu ili kujua maendeleo ya watoto wao na kupata taarifa muhimu zinazowahusu.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Diwani wa Kata ya Vinguguti ambae pia ni Naibu Meya Omar Kumbilamoto wakati alipokua mahafali ya shule ya Sekondari Vinguguti.
Amesema kuwa, ufaulu wa mwanafunzi hautegemei juhudi za walimu pekee bali wazazi nao washiriki kikamilifu kufuatilia maendeleo ya watoto wao.
"Shule za Private mara nyingi wazazi wanapoitwa kupata taarifa za maendeleo ya watoto wao au kujuzwa taarifa muhimu wanafika wote tena Kwa wakati na ikitokea moja hajafika basi anatoa taarifa Kwa Mwalimu Mkuu"amesema Kumbilamoto.
Comments
Post a Comment