MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA WATUMIWA UJUMBE NA JESHI LA POLISI
Na Mwandishi wetu, Dar
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema litaendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ambao unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Taifa wa Benjamen Mkapa Octoba 19, 2024.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amesema kuwa jeshi hilo linaimarisha ulinzi na usalama kabla na baada ya mchezo, hivyo hakutakua na fursa ya mashabiki kuweza kufanya fujo uwanjani.
Aidha, amesema kuwa, hataruhisiwa Askari Polisi yoyote ambae hajapangwa katika eneo maalum kuingia na silaha uwanjani ili kuepusha purukushani yoyote inayoweza kujitoka ni bora kuzingatia maagizo yanayotolewa na jeshi la Polisi.
"Kama ambavyo hataruhisiwa shabiki yoyote kuingia na silaha aina yoyote katika uwanja, basi pia hivo hivo hataruhisiwa Askari yoyote kuingia na silaha ambae hajapangwa "amesema SACP Muliro.
Hata hivyo, amesema magari yarakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni yale ambayo yanatumia card tu, hivyo ambao wahatumii card watatafuta sehemu ya kupaki magari Yao.
Sambamba na hayo, mashabiki wa timu zote mbili wametakiwa kukubaliana na matokeo yoyote yatakayotokea ikiwa ni kushindwa ama kufungwa ilikuepusha vurugu zisizo za lazima.
Katika hatua nyengine amesema zoezi la uandikishaji daftari la mpiga kura linaendelea vizuri mwitikio umekua mzuri,huku akiwataka wananchi kutumia haki yao ya kikatiba ya kujiandikisha ili kuweza kuchagua viongozi ambao wanawataka Kwa kumujibu wa sheria na kanuni.
Comments
Post a Comment