WATU 58 WADAKWA NA KILO 1.066.1 ZA DAWA ZA KULEVYA
Na Mwandishi wetu Dar MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa kukamata Kilogramu 1,066.105 za dawa za kulevya, Milimita 447 za dawa tiba zenye asili ya kulevya huku watuhumiwa 58 wakikamatwa. Dawa hizo zimekamatwa katika oparesheni iliyofanywa na mamlaka hiyo kwenye maeneo mbalimbali nchini kati ya Oktoba na Novemba 2024. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamishna Jenerali DCEA, Aretas Lyimo amesema katika oparesheni hiyo jumla ya ekari 157.4 za mashamba ya bangi na lita 19,804 za kemikali bashirifu zimeteketezwa. Amesema kati ya dawa hizo za kulevya zilizokamatwa, kilogramu 687.3 ni za skanka na kilogramu moja ya hashishi zilizokamatwa eneo la Goba jijini Dar es Salaam zikiwa zimefichwa ndani ya nyumba ya mtuhumiwa. Aidha amesema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, mamlaka ilikamata milimita 120 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Codein zikiwa zinasafirishwa kwenda nje ya nchi pamoja na mil