WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI NA UWEKEZAJI 2024.









  Picha mbalimbali za matukio katika Mkutano wa kimataifa wa madini na uwekezaji Tanzania

Na Mwandishi wetu 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji Tanzania, kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unawakutanisha wadau wa madini wanaojishughulisha na utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji, uongezaji thamani madini, wasimamizi wa Sekta kutoka Serikalini, watoa huduma migodini na wafanyabiashara.

Pamoja na malengo mengine, mkutano huo umelenga kuweka mipango ya kuvutia uwekezaji  wa nje ya nchi, kukuza usimamizi bora wa rasilimali za Madini pamoja na kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Kaulimbiu ya mkutano huo ni _Uongezaji wa Thamani ya Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi_

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...