NLD KUTIKISA UBUNGO LEO, KAMPENI ZA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA



Leo tarehe 25 Novemba, saa 10 jioni, viwanja vya Kwakomba, Mtaa wa King'ongo, Ubungo, Jijini Dar es Salaam, Chama cha NLD kitakuwa na mkutano mkubwa wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mtaa.

Viongozi wa NLD wilaya ya Ubungo wanachukua fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa wilaya ya Ubungo kwenye mkutano huo wa kumnadi mgombea wa Chama cha NLD Mtaa wa King'ongo, Mhe. Patriki Hilaly Ngayungwa.

Pia mkutano huo utaudhuriwa na viongozi wa NLD kutoka makao makuu, kwa lengo la kuunga mkono na kutoa sapoti kwa mgombea wa Chama hicho.

Chama cha NLD kinaendelea na mikutano mbalimbali ya kampeni nchi nzima, huku viongozi wake wakisisitiza kusimamisha wagombea wenye ushawishi katika kila mtaa, kijiji, na kitongoji. Uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji unatarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, nchi nzima.

Comments

Popular posts from this blog

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI