AAT YAFANYIA KAZI MAELEKEZO YA SERIKALI, YATOA WITO HUU KWA WAZAZI
Na Mwandishi wetu
Serikali imeelekeza elimu ya usalama barabarani ianzie kutolewa katika shule ya msingi ili watoto wakue wakitambua sheria za usalama barabarani kwa lengo la kujilinda kutokana na ajali za barabarani hali itakayosaidia kujilinda wanapovuka.
Wadau mbalimbali wameshirikiana ili kuona haki za mtoto zinalindwa hasa anapokua barabarani, ambapo wameanzisha mradi wa kuwajengea uwezo watoto wa shule za msingi ili kujua mahala sahihi pa kuishi wanapokua barabarani
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Wakili mwanasheria wa kikosi cha Usalama Barabarani, ambae pia ni Makamo wa Rais wa Chama Cha mbio za magari Tanzania (AAT) Deus Sokoni
wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Alhasan Mwinyi iliyopo Kinondoni.
Awali miradi huo ulikua ikifanywa na wadau mbalimbali lakini AAT wakaona ni vyema kwenda kwenye shule mbalimbali ambapo wameanza Wilaya ya Temeke na sasa wapo kinondoni kwa kushirikiana na kikosi cha usalama barabarani wanarejea kwenye maelekezo ya Serikali kwamba elimu ya usalama barabarani ianze shule za msingi.
Amesema kuwa, ili kuondoa ajali ambazo ni changamoto kwa watoto wanapotoka nyumbani kwenda shule na wanapotoka shule kwenda nyumbani, wadau wamekubaliana kwa pamoja kutoa elimu hiyo itakayowasaidia watoto hao kuweza kujilinda na kujiepusha na ajali.
Wengine wanabebwa kwenye vyombo vya usafiri magari, wengine wanabebwa kwenye pikipiki na kwa bahati mbaya wazazi wanajiunga wanne au watano, kuwapakia watoto wao kwenye pikipiki alfajiri jambo ambalo si sahihi ni kosa kisheria kwani hata inapotokea ajali mtoto mwenyewe hawezi kujilinda, hatari sana"
Amesema kuwa, mbali na elimu ya usalama barabarani wanayowapa watoto kujilinda wanapokwenda shule, kujiepusha na ajali wanawaelimisha, lakini pia wanawakumbusha wazazi si sahihi mtoto mdogo chini ya umri wa miaka 9 kubebwa katika pikipiki kama abiria , mtoto anapata ajali si rahisi kujilinda yeye mwenyewe, hivyo wanawafundisha watoto wasikubali kubebwa zaidi ya wawili au watatu kwenye pikipiki.
Pia mbali ya usalama barabarani lakini pia wanawaelimisha juu ya haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kulindwa wanaambia kabla hawajaharibiwa, watoto wamuepuke yule ambae anakusudia kumuharibu ni jinai mtoto akatae, inawezekana mtoto akarubuniwa kutokana na shida ya usafiri kwani wapo watu wazima ambao wana nia ovu.
Aidha,wameishukuru Wizara ya Maendeleo Jamii Jinsia Wazee na Watoto, imeliona hilo na imeanza kufanya hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja jukumu la kuelimisha watoto pia na watumiaji wa vyombo vya usafiri watambue haki za watoto, hivyo sheria za barabarani zikizingatiwa vyema watoto wetakua salama.
Ameongeza kuwa, unyanyasaji wa kijisnia wa aina yoyote haukubaliki, watoto wanalawitiwa wanabakwa na madereva wana magari pikipiki ndio maana wamekubaliana na kushauriana na Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini LATRA , katika vyombo vya usafiri mabasi ya usafiri ya watoto lazima kuweza na matroni wa kike lengo ikiwa ni kumlinda yule mtoto na madhila yatakayomuathiri kisaikolijia.
Kwa upande wake, Meneja Kukuza Biashara kutoka AAT Athumani Kassanga amesema miradi hiyo inakuja na ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo AAT ambapo wote kwa pamoja wanajukumu la kulinda uhai wa mtoto anapotumia barabara, wakati anapokwenda shule ama anaporudi nyumbani.
Amesema kuwa, wamekua wazunguma shule mbalimbali za msingi ili kutoa elimu ya usalama barabarani Kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani lengo kutoa elimu hiyo kuanzia ngazi ya chini kama Serikali inavyoelekeza katika kulinda haki za watoto na uhai wao.
"Tumekuwa tukienda katika mashule mbalimbali kuangalia hali ya miundombinu na kujenga barabara zenye alama (Zebra cross) kwa kushirikiana na kikosi cha usalama huku tukitoa mafunzo namna ya kutumia barabara ili watoto wetu wasipate changamoto yoyote wanapokuepo barabara ikiwemo ajali"
"Sisi kama taasisi inayojihusisha na michezo ya magari burudani hii inafundisha watoto kujua nidhamu ya vyombo moto hususani magari na kuwatoa katika michezo hatarishi " amesema Athumani.
Ameongeza kuwa, pia elimu ya usalama mashuleni na wamefanya ni kwa mara ya 3 ambapo hufanya kila mwaka na tayari wameshafikia shule saba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo kikosi cha usalama barabarani.
Aidha pamoja na kuwafikia watoto pia wamefanikiwa kuwafikia bodaboda zaidi ya 5000 kuwapatia elimu huku wakiwapatia kofia ngumu (Helmet) na vifaa vingine vya kufanyia shughuli zao bure.
Comments
Post a Comment