TANZANIA YAENDELEZA KUKUZA SEKTA YA MADINI

 Published from Blogger Prime Android App

DAR ES SALAAM.

Serikali ya Tanzania inaendelea na juhudi za kuimarisha sekta ya madini na kuvutia wawekezaji, huku ikilenga kufanya nchi hiyo kuwa kitovu cha uwekezaji wa madini barani Afrika. Katika juhudi hizo, serikali inatambua kuwa sekta ya madini ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na hivyo inajitahidi kuhakikisha kuwa Tanzania inachangia kwa kiwango kikubwa katika uchumi wa dunia kupitia rasilimali za madini.

Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini, ambao unatarajiwa kufanyika Novemba 19,2024 Katika Kituo wa kimataifa wa Mikutano(JNICC) jijini Dar es salaam, unalengo la kuhamasisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Pia ni sehemu muhimu ya mikakati ya serikali. Kupitia mkutano huo, Tanzania inalenga kuongeza fursa za uwekezaji katika maeneo yote ya mnyororo wa thamani wa madini, kuanzia utafiti, uchimbaji, usafishaji, na uongezaji thamani hadi kufikia masoko ya kimataifa. 

Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Uongezaji Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii" ikihakikisha kuwa rasilimali za madini zinaongeza thamani hapa nchini, badala ya kuondoka zikiwa hazijawa na thamani kubwa.
Published from Blogger Prime Android App
Hayo yamebainishwa leo Novemba 15, 2024 na Naibu Waziri wa Madini katika kipindi cha radio ya Jiji (city fm) jijini dar es salaam Dkt. Steven Kiruswa, amabapo amesema kuwa serikali imeweka mikakati madhubuti ya kuongeza kiwango cha utafiti wa madini, ambapo hadi sasa ni asilimia 16 tu ya eneo la nchi limefanyiwa utafiti wa kina. Lengo ni kuongeza kiwango hicho hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030, ili kuhakikisha Tanzania inapata manufaa zaidi kutoka kwa rasilimali zake. Serikali pia inajivunia kuwa na madini ya kimkakati kama graphite, nickel, cobalt, na lithium, ambayo yana uwezo mkubwa katika kukuza uchumi na kuchangia nishati safi duniani. Kwa kuzingatia umuhimu wa madini haya, serikali imetunga sheria za kuhakikisha kwamba wawekezaji wa madini ya kimkakati wanapaswa kuonyesha mpango wa kuyaongezea thamani hapa nchini kabla ya kupewa leseni ya uchimbaji.

Wachimbaji wadogo, ambao wanachangia asilimia 40 ya pato la taifa katika sekta ya madini, pia wanapata msaada kutoka kwa serikali. Programu kama Mining for Brighter Tomorrow (MBT) zimeanzishwa ili kuwasaidia wachimbaji wadogo, hasa wanawake na vijana, kwa kuwapa mbinu bora za uchimbaji na kuwasogezea masoko ya madini. Serikali pia imeongeza juhudi za kuimarisha masoko ya madini na kudhibiti utoroshwaji wa madini, kupitia masoko 43 na vituo vya ununuzi 105 vilivyopo nchi nzima. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa madini yanauzwa kwa njia halali na mapato yanarejea serikalini.

Kwa upande wa wanawake, serikali inaendelea kuwahamasisha kuwa na ufanisi zaidi katika sekta ya madini. Wanahimizwa kuunda vikundi vya uchimbaji na kumiliki leseni, na tayari mikakati maalum imetengwa ili kuhakikisha wanapata fursa zaidi. Hii ni pamoja na kutoa mikopo kupitia asilimia 10 za halmashauri na mikopo nafuu kutoka kwa benki.

Published from Blogger Prime Android App
Chemba ya Migodi Tanzania (TCM), inayoshirikiana kwa karibu na serikali, inafanya kazi muhimu katika kuhakikisha sekta ya madini inakuwa kwa ufanisi na kwa njia endelevu. Katibu Mtendaji wa TCM, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, alieleza kuwa TCM ni shirikisho la wachimbaji wakubwa na wa kati katika sekta ya madini, na kazi yao ni kuhamasisha uwekezaji na kuunganisha wadau muhimu katika sekta hii. "TCM ina jukumu la kutoa taarifa muhimu kwa wanachama wake na kuhakikisha wanachangia kikamilifu katika utekelezaji wa sera za serikali," alisema Mhandisi Mchwampaka.

Mhandisi Mchwampaka aliongeza kuwa mkutano wa kimataifa wa uwekezaji ni jukwaa muhimu kwa makampuni makubwa ya madini kutambua fursa zilizopo nchini na kuchangamkia uwekezaji katika sekta hii. TCM ina mchango mkubwa katika kuhamasisha uongezaji thamani wa madini na kuimarisha ushirikiano kati ya wachimbaji wakubwa na wadogo. "Tunashirikiana na serikali kuhakikisha kuwa mazingira ya kibiashara ni rafiki, na pia kuhamasisha wachimbaji wa madini kuongeza thamani ya madini hapa nchini badala ya kusafirisha raw materials," alisisitiza Mhandisi Mchwampaka.

Kwa ujumla, sekta ya madini inazidi kuwa tegemeo kubwa kwa uchumi wa Tanzania, na serikali inaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinanufaisha taifa kwa njia endelevu na inayozingatia maslahi ya Watanzania. Juhudi hizi za kuimarisha uongezaji thamani wa madini na kuvutia uwekezaji ni muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania wote

Comments

Popular posts from this blog

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI

TMA YATOA TAHADHARI KUHUSU UWEPO WA KIMBUNGA "HIDAYA"

HUU NDIO USHAURI WA TMA KWA SEKTA HIZI ...