WADAU WA MADINI 1500 KUSHIRIKI MKUTANO WA UWEKEZAJI




Na Mwandishi wetu, Dar 

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Madini imeandaa mkutano wa sita wa  uwekezaji ambao umelenga kuwakutanisha wadau wa madini 1500 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo Mawaziri wa madini kutoka nchi za Afrika, watendaji wakuu wa kampuni kubwa za wauzaji wa madini duniani zilizoekeza na zinazotarajia kuekeza nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema Mkutano huo utafanyika Novemba 19 jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa kimataifa Julius Nyerere, ambapo pamoja na mambo mengine kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameiwezesha Sekta hiyo kupiga hatua kubwa jambo ambalo limevutia wawekezaji wengi.

Amesema kuwa, Serikali ya Tanzania inafanya mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini kila mwaka ili kuimarisha mazingira ya uwekezaji na kuendelea kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo mkuatano huo ni Jukwaa la kujadili kwa pamoja mustakabali wa sekta ya Madini kushirikishana maarifa ujuzi na kuongezea fursa mpya zinazojitokeza katika sekta hii.

Amesema kuwa, mkutano huo ni muendelezo wa mikutano mengine iliyotangulia tangu kuanza kwake mwaka 2019, ambapo serikali ilitenga karibu saa sita kuskiliza kero, changamoto na maoni kutoka kwa wadau wa madini.

"Kutokana na matokeo ya mkutano ule, Serikali imeona kuna umuhimu wa kueka mikutano kama hii yenye sura ya kimataifa ambapo imevuka mipaka ya nchi yetu ikihusisha wadau husika katika mnyororo wa thamani kutoka nje ya nchi"amesema Waziri Mavunde.

Amesema kuwa, nchi ya Tanzania imejaliwa utajiri wa aina mbalimbali ya madini kutoka karibu makundi yote ya madini ikiwemo madini ya metali, madini mkakati, madini ya viwandani, Vito vya thamani kubwa ambavyo vinaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi inayotegemewa kwenye uzalishaji wa madini duniani.

Aidha, amesema Serikali kupitia Wizara ya Madini imeona upo umuhimu wa kuwa na Jukwaa moja linalowaleta wadau kutoka pande zote kusikia kutoka kwao moja kwa moja, kuwepo kwa rasilimali hizo kama zitatumika vizuri zitaweza kuibadili vizuri kiuchumi na kijamii nchi ya Tanzania na kuifanya kuwa nchi inayozalisha madini kwa wingi duniani.

Pia unatoa fursa kwa washiriki kuweza kujifunza sera na mikakati mipya ya Serikali kujadili masula ya kisheria ya kiuchumi yanayohusisha madini na kushuhudia teknolojia mpya ya ubunifu ili kuweza kuleta thamani zaidi kwenye utafiti, uchimbaji na thamani kwenye madini kupitia mawasilisho na mabanda ya maonesho .

Sambamba na hayo, mkutano huo pia unalenga si tu kuvutia wawekezaji bali pia kuweka msingi thabiti wa ushirikiano baina ya wadau kuimarisha uzalishaji wa madini na kuhakikisha kuwa rasilimali hizi zinawanufaisha watanzania kiuchumi na kijamii.

Hata hivyo mkutano huo utaambata na hafla ya usiku wa madini ambapo ni tukio maalum la kutambua mchango wa wadau waliofanya vizuri katika sekta ya madini kupitia makundi mbalimbali pia umelenga kutambua maendeleo ya wadau katika ukuwaji wa sekta huku ikihamasisha wadau wengine waongezeje juhudi kuziona fursa zilizopo na kuchangia mafanikio katika sekta ya madini nchini.

Pia utambatana na onesho la bidhaa za madini ya vito ambapo kwa mara ya kwanza wataachana na utamaduni wa kuonesha madini ya vito pekee na kutokana na kauli mbiu yao watagusa pia aina nyengine ya madini ikiwemo madini ya viwandani lengo ni kuonesha fursa zilizopo na kutambua matumizi ya madini katika maisha ya kila siku ya kiuchumi na kijamii.

Pia mkutano huo utahusisha watafiti, mabalozi 31 kutoka nchi zinazowakulisha Tanzania, wafanyabiashara, taasisi za kifedha, mashirika ya kimataifa, waongezaji thamani madini, vyuo vikuu na vyuo vya kati taasisi za Umma na binafsi, Pia kutakua na mada nane zitakazojadiliwa huku watoa mada wapatao 20 watatoka nje ya nchi na 35 kutoka nchini walibobea katika masula ya madini.

Mkutano wa mwaka huu unaongozwa na kauli mbiu isemayo uongezaji thamani madini, maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambayo inalenga kuhimiza umuhimu wa uongezaji thamani madini kama njia ya kuleta faida kiuchumi na kijamii Kwa maendeleo endelevu ya taifa la Taifa na Dunia kiujumla na kupandisha thamani madini yanayozalishwa nchini kabla ya kusafirishwa nje Kwa lengo la kuchochea uanzishwaji viwanda vitakavyokuwa na manufaa nchini na majirani wanaotunguka.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI