AZAM MEDIA YAWAPA WATEJA WAKE OFA HII, YAZINDUA TAMTHILIA 3 KWA MPIGO
Na Mwandishi wetu, Dar KAMPUNI ya Azam Media Ltd kupitia msimu huu wa sikukuu ya Christmas imezindua tamthilia tatu kwa mpigo ambazo zinakwenda kutoa elimu kwa watazamaji wake sambamba na kuwapatia burudani isiyo kifani na kukonga nyoyo zao. Akizungumza Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo Msimamizi Mkuu wa chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza amezitaja tamthilia hizo kuwa ni Kombolea, Tufani pamoja na Kiki ambazo zimeandaliwa kwa ubunifu mkubwa. "Tamthilia ya Tufani itaanza kuonyeshwa Desemba 9,2024 kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi saa 1:30 usiku,Kombolela itaanza kuonyeshwa Disemba13,2024 siku ya ,ijumaa hadi jumapili saa 1:00 usiku,huku tamthilia ya Kiki itaanza kuonyeshwa Desemba 16 ,2024 jumatatu hadi Alhamisi saa 1:00 usiku,ambapo tamthilia zote hizi zitaonekana kupitia chaneli namba 106 Sinema zetu HD" amesema Mgaza Nakuongeza kuwa" Lengo la Azam Media Ltd kuendelea kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji Wetu huku tukisukuma Sanaa yetu ...