UVCCM KIJANI AWARDS 2024/2025: DIRISHA LA KUJISAJILI LINAKARIBIA KUFUNGWA
Dirisha la usajili kwa ajili ya kushiriki katika UVCCM Kijani Awards 2024/2025, tuzo za kihistoria zinazolenga kutambua juhudi za vijana wa Kitanzania katika kuleta mabadiliko chanya, linaendelea kufungwa tarehe 10 Januari 2025 saa sita usiku.
Zikiwa zimebaki siku nne tu, vijana kote nchini wanahimizwa kuchangamkia fursa hii adhimu ya kuthibitisha uwezo wao wa kuwa viongozi wa leo na kesho. Tuzo hizi, zinazotolewa kwa mara ya kwanza, zinawapa nafasi washiriki kuonesha juhudi na mchango wao katika jamii kupitia ubunifu, uongozi, na mshikamano wa kizalendo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji wa tuzo hizo, vijana wanaotaka kushiriki wanapaswa kutembelea tovuti rasmi ya UVCCM Kijani Awards kupitia www.uvccmawards.or.tz, kujaza fomu zao kwa umakini, na kuthibitisha taarifa zao kabla ya muda wa mwisho.
"Huu ni wakati wa vijana kuandika historia. Hatutaki kuona mtu yeyote anayepoteza nafasi hii muhimu ya kuwa sehemu ya washindi wa kihistoria wa Kijani Awards. Tuzo hizi ni jukwaa la kuonesha vipaji, bidii, na maono ya vijana kwa ajili ya maendeleo endelevu ya taifa," amesema Spesho Kabwanga.
Kwa wale ambao bado hawajajisajili, ujumbe ni wazi: Usisubiri dakika za mwisho. Chukua hatua sasa na thibitisha nafasi yako katika historia ya tuzo hizi!
Kwa maelezo zaidi na kujisajili, tembelea tovuti www.uvccmawards.or.tz.
#JumuiyaYetuNdotoYetu
#UVCCMKijaniAwards24
Comments
Post a Comment