KILWA YARINDIMA SIKU YA WAPENDANAO DUNIANI.




Ni mwendo wa Shamrashara za watalii ndani ya TAWA SEA CRUISER

Siku adhimu  Kwa ajili ya kuwakutanisha wapendanao almaarufu Valentine's Day inaendelea vyema ndani ya Hifadhi ya urithi wa utamaduni wa dunia ya Magofu ya Kale ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambapo watalii kutoka sehemu mbalimbali wapo ndani ya Hifadhi hiyo wakisheherekea Kwa kubarizi ndani ya boti la kisasa lijulikanalo Kwa jina la TAWA SEA CRUISER 

Kadri muda unavyosonga ndivyo Idadi ya watalii inavyozidi kuongezeka kwa Kasi na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kupitia Hifadhi hiyo  inatarajia kupokea  wageni  wengi  siku ya leo kutokana na mvuto wa Hifadhi hiyo ambayo hivi karibuni imekuwa ikipokea Idadi kubwa ya watalii kutoka Mataifa mbalimbali duniani na watalii wa ndani.

TAWA inaendelea kuwakaribisha watu wote kutembelea hifadhi hiyo kujionea vivutio vya kihistoria na kiutamaduni ikiwemo kufurahia mandhari nzuri za fukwe pamoja kuona viumbe vya majini kupitia TAWA SEA CRUISER.

Comments

Popular posts from this blog

MALYA ACHUKUA FOMU YA UDIWANI VITI MAALUM

MAKAMO WA RAIS SMAUJATA ATIA NIA UBUNGE KIVULE

NLD YAZINDUA KAMPENI "FYEKA CCM", YATOA WITO HUU KWA TAMISEMI