FAINAL YA KOMBE LA JERRY SLAA CUP YAINGIA DOA, PURUKUSHANI ZA MASHABIKI, REFA AONDOLEWA UWANJANI KWA DIFENDA.
Na Mwandishi wetu
Final ya mechi ya mpira wa miguu ya kombe la Jerry Slaa Cup Kati ya Mazinda na Shelaton United imehairishwa jana baada ya vurugu zilizotokea na kushindwa kufikia muafaka wa timu zote mbili.
Awali timu ya Shelatoni ilishinda mabao mawili katika kipindi cha kwanza cha dakika 45 huku timu ya Mazinda ikiambulia Sifuri.
Kipindi cha pili dakika chache baada ya kurudi uwanjani timu ya Mazinda iliandika bao la kwanza jambo lililopelekea kusimama kwa muda kwa mchezo huo.
Goli la kwanza lililofungwa na timu ya Mazinda lilikataliwa na timu ya Shelatoni United kwa madai kipa wao amechezewa rafu na kusababisha timu hiyo kugoma kuendelea kucheza.
Wachezaji wote wa Shelaton United walitoka nje ya uwanjan na kushinikiza refa kukataa goli ili waendelee na mchezo, huku mashabiki wa timu hiyo wakitoa maneno makali kwa viongozi na refa.
Tambo za mashabiki zilichukua muda, huku waliokua mbali na jukwaa kuu wakibaki njia panda wakisubiri hatma ya viongozi, mchezo huo ulisimama kwa zaidi ya dakika ishirini bila kupatikana Suluhu yoyote.
Baada ya muda mrefu timu ya Shelatoni United ilikubali kucheza, na timu ya Mazinda nayo ikagoma kwa madai kuwa muda umeenda hawawezi kuendelea na mchezo kwani uwanja huo hauna taa mchezo hauwezi kuwa fear.
Vuta nikuvute ziliendelea uwanjani kati mashabiki wa miamba hiyo miwili ya Kata ya Buyuni huku wakimzonga refa na maneno ya dhihaka waliyokua wakiyatoa badhi ya mashabiki wa timu ya Shelatoni United .
Kikao cha dharura kikakaliwa kati ya Polisi Kata wa Kata ya Buyuni, makepteni wa timu zote mbili, viongozi wa timu zote na mgeni rasmi aliyeandaliwa kutoa zawadi na kufikia muafaka wa mechi hiyo kughairishwa hadi itakapotangazwa tena huku refa akiondoka na difenda la Polisi uwanjani kwa usalama wake.
Mshindi wa tatu ameshapatikana ni Seven ni Turch, bado mshindi wa kwanza na pili ambapo mshindi wa kwanza atapata Ng'ombe pamoja na Jezi, wa pili atapata mbuzi wawili na mshindi wa tatu atapata mbuzi mmoja.
Comments
Post a Comment